Jamaa analalamika kutongozwa na njemba

Simba Mkali

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
620
Reaction score
239
Kuna mshika mmoja analalamika kutongozwa na wanaume mwenzake, kisa cha yote ni mke wake. mke wa jamaa alienda sokoni na kukutana na mwanaume aliyemtongoza na kisha kumuomba namba ya cm mwanamke akakubali ila akadanganya jina na kutoa namba ya mumewe na kumwambia jamaa nipigie baadaye kwa kuwa sasa hivi haina chaji.
Kila akitongozwa na wanaume mwanamke huyo anafanya hivyohivyo jamaa amenilalamikia kuwa afanye nini kwa kuwa sasa imekuwa too much, jamaa wanapiga kumtongoza na wengine wanakuwa wakali wakisikia sauti ya kiume na wanamwambia " Acha kupokea simu za watu mpe mwenye simu yake." eti afanyeje?
 
Amwambie mke wake aache kutoa namba yake, kama kuliwa anaweza kuliwa tu na siku akiliwa hatajua aache kumzuga kwamba ni mwaminifu sana.
 
Amwambie mke wake aache kutoa namba yake, kama kuliwa anaweza kuliwa tu na siku akiliwa hatajua aache kumzuga kwamba ni mwaminifu sana.

the lady is taking an alibi!jamaa atajiona yes mke wangu muaminifu!
 
Amwambie mke wake aache kutoa namba yake, kama kuliwa anaweza kuliwa tu na siku akiliwa hatajua aache kumzuga kwamba ni mwaminifu sana.

Mkuu nakubaliana na wewe anajitia usafi ambao hana, mwanamke asiyetaka kutongozwa hawezi kutongozwa, Ipo sura ya 'no-nonsense' akiweka hata kama ulikuwa umekuja kwa nia hiyo utajikuta unaulizia dada samahani eti sasa hivi saa ngapi! huyu hana neno kabisa anamzuga mume wake tu
 
Amkomesha huyo wife wake hana ulazima wa kutoa namba anaweza kukataa bila ya kutafuta headache nyengine
 
Akutane nae live ili atiwe jambajamba huyo mtongozaji
 
Safi kabisa,mama anaonyesha Kuwa na yeye anatongozwa hivyo punguza umalaya mtaani,huwezi jua huenda rafiki yako anamademu kibao muulize vizuri
 
Amkanye mkewe na hiyo tabia maana nahisi kama ni hujuma vile! Kutongozwa atongozwe yeye iweje namba ya simu atoe ya mumewe? Si angebuni namba yoyote tu kichwani aitoe? Hivi ni lazima kila mwanamke anayetongozwa anatakiwa kutoa namba ya simu? :sleepy:
 
Ana show love kwa husband

Pamoja sana. Tatizo la dada zetu wa kusini Mtwara hawajui kukataa. Hivyo ndiyo kajitahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…