Jamaa kaingizwa chaka na dalali kwenye nyumba ya kupanga

Jamaa kaingizwa chaka na dalali kwenye nyumba ya kupanga

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
5,934
Reaction score
10,206
Kuna bwana mdogo mtoto wa jirani yangu tulikuwa naye hapa Dom alimaliza chuo akakosa ajira ikabidi aje tupige naye mishe za kuuza majeneza angalau apate japo pesa ya kula na tumekuwa naye hapa for almost one year

Sasa week iliyopita amebahatika kupata ajira kwenye taasisi moja binafsi Dar ikabidi aende huko akaanze kazi
Sasa alipofika kuanza kazi akaona sio vyema kuishi kwa washkaji ikabidi atafute chumba cha kupanga na kama mjuavyo kupata chumba au nyumba ya kupanga Dar bila dalali ni ngumu

Sasa kapata dalali akamtafutia nyumba na kumpa sifa kibao kwamba nyumba iko pazuri kuna huduma zote muhimu na pia hakuna wapangaji wengi basi ilikuwa asubuhi ya siku hiyo jamaa akaenda akapaona akamaliza malipo kabisa ili jioni ya siku hiyo ahamie.

Kutokana na uchovu wa mizunguko na yule dalali basi Dogo hakukagua ile nyumba vizuri zaidi ya kuangalia chumba na kusema kinamfaa akalipia kabisa miezi 6.

Picha lilianza ile jioni wakati anakuja kuweka vitu vyake vya ndani ili ahamie rasmi anakutana na makelele ya music nje kuna speakers zinapigwa nyimbo za zamani

Ile anaingia uwani anakutana na walevi wamekaa kwenye mabenchi ya mbao na wengine wamelala chini kabisa hapo ndo akagundua nyuma ya hiyo nyumba ni kilabu cha pombe za kienyeji Yaani yule mama mwenye nyumba anauzaga konyagi mwitu!

Jamaa akaamua kurudi chumbani na kupanga mizigo yake ili ajue cha kufanya sasa kutokana na joto la Dar akaamua akaoge kwanza lakini anauliza lilipo bafu anaelekezwa nyuma ya nyumba kule uani kwa wale walevi bafu na choo ni passport size yaani hata ukichuchumaa watu wakiwa nje wanakuona kuanzia usawa wa kifua na shingo mpaka ulivyokunja sura

Yaani kifupi choo na bafu mnashare na walevi Yaani jamaa alichoka kabisa anatoka anampigia dalali hapatikani halafu mama mwenye nyumba anasema huwa akishapokea hela harudishi!

Kifupi imebidi Dogo aishi tu amalize kodi yake.
 
20250216_162407.jpg
 
Hiv Mkuu mbwa dume kumbe tu bado sponsa wako kwenye biahara yako ni israeli Mtoa roho?🤔
 
Kama kweli, huyo dogo ndo kazingua... yaani kwenye nyumba za kupanga, kitu cha kwanza kabisa kuangalia ni choo... lakini inawezekana aliamua kulipa haraka haraka labda aliambiwa kodi ni elfu 15 au 20...
 
Sasa ukienda kupanga si lazima uoneshwe hayo yote kabla hujalipa
I mean uone chumba,wapi utapata maji,na kwa jicho la uchunguzi uangalie hadi duka na kama kama mamanzi wapo mtaani angalau wa kuanzia anzia
Dogo zwazwa... yeye sijui alikuwa anaangilia nini?? Yaani vitu vyote vya msingi inaonekana hajakagua
 
Unapoenda kupanga uswahilini yaani ukishaangalia chumba ukaridhika nacho fasta upelekwe uone maliwato.
Madalali huwa na maneno mengi sana sio wa kuwasikiliza sana, we angalia vigezo vyako.

Na huyo dogo kalipia bei gani isihekua kalipia 25k kwa mwezi halafu ni magomeni na analalamika choo ni passpodt size.
 
Back
Top Bottom