Kichwa Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 1,726
- 314
Mnaokoa ndoa gani? Hvi umuhimu wa ndoa ni watu kuishi nyumba moja au ni kuheshimu yale makubaliano mliyowekeana toka mwanzo? Tangu hapo hakuitaka ndoa ndiyo maana alitoka nje. Hata mrembe, mpake asali ukweli unabaki pale pale huo ni uovu. Kikubwa ni kubadili tabia na kuacha kuficha uovu! Neno la Mungu linasema Chachu kidogo huchachua donge zima.Hakuna anayefundisha mtu uovu hapo...watu wanajribu kuokoa ndoa hapo! Ngoja yakukute ndio utaona umuhimu wa kupata ushauri humu.
Hizi ni stori za kutunga!!halafu hizi stoey zako kaka vipi...hutungi kweli...kuna hii hapa
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/122733-nitawezaje-kukabiliana-na-majaribu-haya.html
kwa hii post niliyoweka link naona kama halmashauri ya ubongo wako iko hovyo
Ahahahaah!! Kigogo umeuwa!kama ni mimi nakataa kabisa kuwa meseji ni yangu ..ntamwambia mama gaude wangu kuwa unajua mitandao hii ya simu na mapromosheni haya network zinaingiliana unakuta meseji zikiwa hewani zinapotea njia maana mkongo wa mawasiliano wa taifa unazidiwa sasa kwa kuwa simu yako hutumi tumi meseji ndo maana zinakuja kwako maana inbox in nafasi..lakini tupige huko Tigo tuwaulize meseji hii imetoka wapi....nikimaliza utetezi wangu navuta cocacola baridi naendelea kuangalia TV kipindi cha mzee wa upako ...issue imeisha hapo
Mmmmh!
Nyie wanaume mpoje lakini?
Amwambie alimuazima mtu simu yake na hajui alichokifanya.
Akishindwa aseme ukweli kuwa alilala na mwanamke mwingine.
Za mwizi arobaini. Nae amezidi.
Bichwa lake.
Kama hujao useme wewe ndiye uliandika hiyo sms kwenda kwa mtu wako, kama umeoa tafuta jamaa yenu ambaye hajaoa aseme yeye ndiye aliandika kwa mtu wake. Illa mwambie huyo jamaa yako aache ufenenge, mtu ana mke mzuri hivyo halafu aenda kwa Vibiriti Ngoma!!
halafu naona kuna watu wanaleta story kisha JF wanajadili, kuna siku watu watatunga hadith kutoka na mawazo ya wengine.. wtachakachua stori zooote , copy, paSte, edit, mara kitabu hichoo....mhhhhh JF bwana, I LOVU UHizi ni stori za kutunga!!
Hata wadada nao wanajifunza uongo kupitia humuhumu!Kumbe waume zetu uongo hujifunzia hapa JF
Kwamba kuna wanaume ni aibu kuwaita wanandoa maana ni wanaDOA!Husninyo, D A, Lizzy etc Mwajifunza nin toka ktk hz threads? teh! teh!
good Idea...akubali hasara,tena hiyo simu ispatikane tena.Hapo hakuna ujanja labda apoteze simu na ajitetee kuwa hiyo meseji imetumwa na wezi wake wa simu..
Hata wadada nao wanajifunza uongo kupitia humuhumu!
Ama kweli za mwizi arobaini, nikiwa naendelea na kazi zangu humu ofisini kuna rafiki yangu mmoja amekuja ofisini kwangu macho yamemtoka, sijamuuliza tayari akanipa simu yake na kunionyesha sms ambayo kwa wakati huo ilikuwa bado ipo juu ya screen. Aliposcroll hadi chini nikaona ni jina na namba ya mke wake. Ujumbe ambao uliforwadiwa na mywife wake uliandikwa hivi: "SIKUTEGEMEA KAMA UNA MAPENZI MATAMU NAMNA ILE, YAANI JANA NIMELALA MWEPESI NA HATA KWENYE NDOTO ZANGU WEWE NDO ULITAWALA, NAAHIDI SITOKUACHA DEAR!". Sababu ya kuja kwangu mbio ni kunieleza kosa alilofanya na kuniomba ushauri ili akakabiliane na mkewe nyumbani. Nimebaki nacheka ingawa jamaa anataka kulia na nikamuahidi tukapate lunch pamoja ili tuchakachue ishu. Nimshauli vipi jamaa huyu ili wainusuru ndoa yao?
...panic ya nini, kwani jana hakulala kwake? amwambie ndio kamtumia yeye (mkewe) ujumbe huo.
Tena mwambie akakamae na kumkazia macho wakati akiyatamka hayo iwapo atashindwa mkumbatia.
Na kama hakutoa huduma kwa wife siku hiyo asemeje?:disapointed:
Ama kweli za mwizi arobaini, nikiwa naendelea na kazi zangu humu ofisini kuna rafiki yangu mmoja amekuja ofisini kwangu macho yamemtoka, sijamuuliza tayari akanipa simu yake na kunionyesha sms ambayo kwa wakati huo ilikuwa bado ipo juu ya screen. Aliposcroll hadi chini nikaona ni jina na namba ya mke wake. Ujumbe ambao uliforwadiwa na mywife wake uliandikwa hivi: "SIKUTEGEMEA KAMA UNA MAPENZI MATAMU NAMNA ILE, YAANI JANA NIMELALA MWEPESI NA HATA KWENYE NDOTO ZANGU WEWE NDO ULITAWALA, NAAHIDI SITOKUACHA DEAR!". Sababu ya kuja kwangu mbio ni kunieleza kosa alilofanya na kuniomba ushauri ili akakabiliane na mkewe nyumbani. Nimebaki nacheka ingawa jamaa anataka kulia na nikamuahidi tukapate lunch pamoja ili tuchakachue ishu. Nimshauli vipi jamaa huyu ili wainusuru ndoa yao?
Nazeeka vibaya huo ujumbe uliforwadiwa na mkewe kutoka wapi?? Nisamehe sijui njaa kama sijaelewa