Jamal Malinzi: Uchu wa madaraka utakutumbua

SONGOKA

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
1,841
Reaction score
1,843
ukiyashangaa ya amboni utayaona ya gamboshi

Ndugu Jamal Malinzi kachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha mpila wa miguu mkoa wa KAGERA. Whaaaat, Jamal Malinzi Rais wa TFF kachaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa KAGERA.

Hata kama katiba inaruhusu, hivi busara umeiacha wapi kaka yangu malinzi?? Mambo ya TFF yenyewe yanaenda mrama, mali za shirikisho zinashikiliwa na TRA, Kocha wa Timu ya Taifa hajalipwa miezi kibao, Uwanja wa taifa haufanyiwi renovation, Lakini bado your comfortable kugombea tena uenyekiti wa mkoa. SERIOUSLY

Tatizo mlangu liko hapa
  1. kwanza huu utaratibu ni conflict of interest, wewe kama RAIS linapokuja swala la mkoa wa KAGERA katika ofisi yako tuna uhakika gani kama hakutakuwa na upendeleo. Kwa mfano vigezo gani vilitumika katika kufanywa major renovation uwanja wa kagera na ukaachwa uwanja wa KARUME musoma foristance??
  2. Mpaka sasa TFF ina matatizo lukuki, kiasi cha kushindwa hata kulipa madeni na mishahara kwa baadhi ya waajiriwa. Huo muda wa nyongeza (spare time) wa kuongoza soka la KAGERA UTAUTOA WAPI, ukuzingatia haya matatizo lukuki ya TFF
  3. Ofisi za TFF ziko DAR, na ofisi za uenyekiti wako wa kagera ziko hukohuko bukoba, Je unatuhakikishiaje kuwa utakuwa unapatikana kufanya shughuli zako za kila siku katika ofisi zote mbili zilizo KM 1000 apart?
  4. Pia tunashindwa kujua, tutatenganishaje matumizi yako ya fedha za umma pale utakapokuwa unatekeleza majukumu ya mwenyekiti wa kagera. Kwa mfano ukisafiri kwenda kagera,
Kuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu TAIFA (TFF) sio jambo loa kitoto, so tulitegemea uachane na hizi habari za kudunduliza tunafasi tusitokuwa na tija kwa taifa.

Ndugu malinzi katika zama hizi za HAPA KAZI tu, Rais ameshakataa mambo ya kushika vyeo mia kwa watendaji wakuu. Hivi unalijua hilo

Balaza la michezo, na waziri @nape , hivi mnaruhusuje huu utaratibu wa ajabu ajabu kuendelea.
 
Tanzania yaani kila sehemu ni shida tu.
 
mim kwa kwel ni sawa rais awe mkuu wa mkoa at the same time.... halfu haoni ikifka muda wa kupiga kura Kwenye uchaguz mkuu wa TFF kagera itakosa mwakilish kwa maana yeye atasimama kama TFF /Mgombea
 
unamaanisha ni mkuu, J malinzi anafungua viwanda vya uongozi??
Ndiyo maana yake sasa Unaitwa rais wa nchi ukawe tena mkuu wa mkoa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Huyu jamaa haishiwi vituko. Hapa inajionyesha kwamba hana uhakika wa kuendelea na Urais wa TFF.
 
Kajiandaa kushindwa uchaguzi wa TFF mwakani anajua keshaboronga na haweiz kurudi pale TFF kutokana na madudu alioyafanya
 
Ndiyo maana yake sasa Unaitwa rais wa nchi ukawe tena mkuu wa mkoa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
ha ha ha ha kweli hii nchi ya VIWANDA MWENDOKASI
 
Ndiyo maana yake sasa Unaitwa rais wa nchi ukawe tena mkuu wa mkoa[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Naam, hii nayo yawezekana Rais wa Jamhuri ya Tanzania na Mwenyekiti wa CCM-Taifa akaenda kugombea Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita. Malinzi anatafuta kuharibu soka la Tanzania
 
Sasa ili na sisi wanakagera tusikuone ovyo bw.Jamal malinzi chonde chonde amishia makao makuu ya TFF mjini Bukoba daima tutakua pamoja na wewe...
 
Naam, hii nayo yawezekana Rais wa Jamhuri ya Tanzania na Mwenyekiti wa CCM-Taifa akaenda kugombea Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita. Malinzi anatafuta kuharibu soka la Tanzania
hivi taratibu za kumtumbua Rais wa TFF ni zipi
 
hivi taratibu za kumtumbua Rais wa TFF ni zipi
Mzee hawa jamaa wamejiwekea wigo mkubwa wa kujilinda na kulinda madaraka yao. Nakumbuka jinsi watu walivyopigana kumtoa Ndolanga. Ilikuwa balaa, watu walikesha ukumbini na ukumbi pamoja na mahoteli walipofikia wajumbe walijazwa mashushu ili kufanikisha lengo la kumtoa madarakani.
 
Acheni wivu wa kike, nyie kama hamna vyeo mwenzenu amevipata.
 
Sio kama kuwa rais lazima uwe Mwenyekiti wa mkoa?? Kama ilivyo waziri kuwa mbunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…