Kada machachari wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Jamal Mangu, leo Juni 29, 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Nyang’hwale, lililopo wilayani Nyang’hwale, mkoa wa Geita.
Komredi Mangu amesema amejiandaa kwa dhati kulitumikia jimbo hilo kwa kusimamia maendeleo jumuishi na kushirikiana na wananchi katika kujenga ustawi wa jamii.