Jamani aliewahi kutumia tretinoin

Jamani aliewahi kutumia tretinoin

ms emmaa

Senior Member
Joined
Jun 13, 2023
Posts
119
Reaction score
207
Naomba mrejesho kwa alotumia tretinoin na positive and negative effects zake
 
Naomba mrejesho kwa alotumia tretinoin na positive and negative effects zake
Mimi binafsi nilikuwa ninachunusi, ila zinakuja na kuondoka yaani sio serious kivile, mwaka huu mwezi wa kwanza mwishoni zikaanza chunusi very serious, uso mzima mpk shingoni na kifuani halafu kubwa kubwa, nikaenda kwa madaktari wa kawaida nikapewa salicylic acid with betamethasone, nikapaka lakini ile dawa haikuondoa chunusi, ilinichubua nikawa mweupe mpk nikaogopa 😂, nikaamua tu niende kwa specialist pale rabininsia, nikapewa hio dawa TRETINOIN, DOXYCYCLINE, BENZOYL PEROXIDE na HYDROCORTISONE, nikaambiwa nitumie kwa mwezi mzima then nirudi, cha ajabu nimetumia hizo dawa kwa wiki 1, chunusi zikapotea kabisa, yakabaki makovu meusi lakini uvimbe hamna, hapa navyoandika ni wiki ya pili na nusu, makovu yameisha yote, yaani nipo smooth kama sijawahi kupata chunusi 😂😂😂,

Kuna dawa sikuzitumia kutokana na maelezo ya doctor, hydrocortisone niliambiwa nipake pale navohisi nawashwa, kwahiyo niliiacha sikupaka, ila TRETINOIN NI KIBOKO YA CHUNUSI hii dawa inahatari sana kwakweli....

Dosage
Benzoyl peroxide - nilipaka asubuhi tu

Doxycycline - nilimeza usiku tu, kidonge kimoja

Tretinoin- usiku tu, kabla ya kulala, usikae kwenye joto sana itayeyuka, kama unafeni unaweza ukawasha iliidiffuse kwenye ngozi

Hydrocortisone - hii niliambiwa nipake kama nikiwashwa, binafsi sikuwa nawashwa kwahiyo sikuitumia kabisa

Side effects za tretinoin
Ukitumia tretinoin ngozi inakuwa haiwezi kuhimili miale mikali ya jua, hivyo unashauriwa kukaa indoors au matumizi ya sunscreen

Wajawazito marufuku kutumia tretinoin, itakachomfanya mjamzito atakaepaka me mwenyewe sijui 😂
 
Back
Top Bottom