Jamani Babu, Mjukuu hadi Kitukuu

amenyamana

Member
Joined
Sep 19, 2011
Posts
47
Reaction score
5
Kisa hiki cha kweli kimenisikitisha binafsi na hata jamii yetu ya Kiafrika , Kimetokea hapa wilayani Arumeru katika kijiji maarufu kwa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa. Babu amempa mimba mtoto wa mwanae wa kumzaa yaani mjukuu wake wa darasa la sita. Huyo mjukuu alianza huo mchezo na babu yake takriban mwaka moja uliopita, alijifungua wikii iliyopita na baada ya kubanwa na wazazi wake ndipo akasema kuwa ni babu ndiye mhusika wa hiki kiumbe. Babu alipelekwa polisi lakini ndugu zake walihonga kabla kesi haijaenda mahakamani na akapewa dhamani na yuko nje. Je kwa ukatili huu kama jamii tuchukue hatua gani? .Nawasilisha
 
Yaani hata Wameru jamani! Ee Mungu tusamehe tumekukosea sana, ulitujua hata kabla hatujawa tumboni mwa mama zetu, unajua madhaifu ya kila mmoja wetu, Amen!
 
mjukuu mbona yuko mbali?watu wanamega mpk watoto wa kuwazaa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…