Murphy's Law inasema "Anything that can go wrong, will go wrong"
Interpretation nyingine ya hili ni kwamba, kisichokatazwa, kimehalalishwa.
Kwa msingi huo, pengine swali la kuulizwa hapa ni, je, imekatazwa kwa mtu ambaye hana CPA kufundisha CPA review?
Kwa sababu ujue kufundisha si sawa na kufanya, wenyewe wanasema "Those who can't do, teach". Ndiyo maana sio kila mwalimu anaweza kufanya anayofundisha, na sio kila anayefanya anaweza kufundisha.
Kuna mkoa mmoja nimeenda nikakuta kuna watu wanafundisha watu wanaotafuta CPA lakini hao walimu wenyewe hawana CPA, inakubalika hii? Au kama mtu amesoma finance anaijua vyema anaweza kufundisha? au kama mtu ana postgraduate ya taxation anaweza kuwa anafundisha somo la kodi hata kama hana CPA?
wadau mi sielewi, naomba kufaamishwa!