Jamani hawa ma last born watatupasua vichwa!

Mi kabla sijachangia nina maswali haya:
1. Huyo last born ni jinsia gani?
2. Wako watoto wangapi jumla katika familia?
3. Je kuna tofauti ya miaka mingapi kutoka kwa last but one?
Ahsante kwa ushirikiano...
 

hili la bakora vs no bakora ni zito,na hata serikalini mjadala mzito unaendelea hadi leo kama watoto shuleni waendelee kuchapwa au la? fimbo zinasaidia kumjenga mtoto au zinamharibu kisaikolojia? It is a big debate Mkuu,unaonaje ipatikane siku ifunguliwe thread maalum kujadili jambo hili.
By the way unaamini kwa dhati kabisa kuwa umefanikiwa maishani kwa sababu ya bakora? na wanaofanikiwa bila kuchapwa (kama mimi Bishanga?)
 
mtoto umleavyo ndio akuavyo

badilika kitabia katika malezi ya huyo mtoto , unatakiwa mtoto umwelekeze nini anatakiwa kufanya kuanzia asubuhi hadi usiku akitaka kulala .. na naaamini malezi hayana tofauti kati ya first, mid na last born
wewe ni wa ngapi?
 
physical/emotional/mental violence zote ni mbaya,kwa hiyo to you bora physical?
 
una uhakika wewe ndo ulikuwa msikivu kuliko wote? can your sisters vouch for that au unajifagilia Mkuu?
 
heri ya wewe mkuu wako mkubwa walau mnaweza kuelewana. Wangu mie ni kadogo halafu kamejua kuwa ndo mtoto peke yake, yaani kila kitu tunaenda opposite
aisee pole,usikachape lakini,we nenda nako taratibu kakikua katabadilika.
 
Mi kabla sijachangia nina maswali haya:
1. Huyo last born ni jinsia gani?
2. Wako watoto wangapi jumla katika familia?
3. Je kuna tofauti ya miaka mingapi kutoka kwa last but one?

Ahsante kwa ushirikiano...
1.kavulana
2.sita,4 girls,eldest 25,youngest 12
3.Wengine wamezaliwa wawili wawili within the same year mama tofauti.
nimejieleza vizuri?
 
physical/emotional/mental violence zote ni mbaya,kwa hiyo to you bora physical?

Hakuna namna ya violence iliyo bora. nachosema adhabu isitafsiriwe kama ni ukatili. Kwa mfano kwa mimi naeamini katika viboko si kwamba situmii approach zingine la hasha. Nazitumia. Kuna hatua kuna kosa anapofanya mtoto mdomo tu unatosha kwamba bwana ee umekosea sitaki urudie hivyo tena. Akirudia kosa ntamkumbusha na akirudia tena kiboko lazima kipite kuonesha sikubaliani nae.

Lakini nikumbushe hakuna njia inayoguarantee matokeo bora zaidi. Sababu wapo waliochapwa na mwisho wa siku wakaendelea na tabia zao mbaya (kushindikana hadi ukubwani). Wapo ambao hawajachapwa walikua wanaonywa tu kwa kauli na kunyimwa na mzazi vitu (privileges) flani flani na bado wakaharibika (shindikana) hadi ukubwani. So adhabu zote inategemea pia na utayari wa mtoto kuamua kurekebishika. ila kinachoamua matumizi ya adhabu ni historia ya familia (kama mmekua na tradition ya kutumia adhabu hiyo toka mwanzo) na uwezo wenu kifedha (hili la pili ni hisia zangu zaidi)
 

inaoneka ingawa bado hajakuwa; utoto wake ulikuwa unamdekeza mbaya, akifinywa ----------usinifinyie mwanangu; akilia ----------------mtoto umemfanya nini mbona analiia; hebu kamuogeshe mtoto; mtoto amekula; mbona hujamkaangaia mayai; mtoto kakojoa hebu lete tambala ufute; hebu kamuogeshe mtoto, hapo yuko darasa la sita; mtoto kamaliza kula mbona hujatoa vyombo mezani; usinipigie mwanagu sasa kama kakutukana ndio umpige! kwani yeye anajua nini hata ukimpiga;

hayo ni baadhi ya wazazi wanayowambia either mahouse- boy/girls au walezi kwa watoto wao full kuwadekeza, kuwalea kama mayai, matokeo yake akianza kukua mtoto anakuwa kichwa kigumu; kiburi; hajui kazi hata kujifulia chupi yake; sembuse kutoa sahani mezani na huku akijua kuna boi; yote ni matunda ya malezi pengine hata TV chumbani umemwekea iyo homework atafanya saa ngapi naye anawza kucheza game?

Tafakari chukua hatua ; samaki mkunje angali mbichi; hiyo ndio inachangia maadili katika jamii kuzidi kuporomoka.
 

Nakupongeza sana Mkuu ,kwa kweli sina la kuongezea hapa,thanks.
 

bonge la tuition,ahsante Rubi.
 
Mimi ni last born ndugu na ndiyo mtoto wa kwanza katika familiya kuaza life mapema na ninajua nini ninachokifanya,malezi yako kwa mtoto wako yanalete impact hiyo
 
mi ni last born pia,but u dot com ndo unaharibu watoto wengi sana,mpe mboko za kutosha na majukumu yaendayo na umri wake na make sure anatekeleza,jaribu kumjengea ratiba amabayo lazima aifate,mpangie muda wa games,masomo,ku socialize na wenzake na ndugu,kujihusisha na dini na mengineyo,yote yakienda sambamba tutajenga taifa bora,mfano mm by da time nipo form one nilikuwa nikiamshwa saa moja na kupiga deki vyoo vyote na kufagia uwahi before kwenda shule,,mjengee kujitegemea,mjengeee ratiba kamilifu na punguza kuchekacheka nae punde anapofanya upuuzi
 
mimi ni last born na niko vizuri tu wa kulaumiwa hapo ni nyie wazazi kwani hayo magame kayaokota si mmempa wenyewe jamani.
mlee mtoto kwa njia nzuri bwana wala hataicha hadi atakapokuwa mzee
ahhhhhhhhh,kumbe ni last born???
 
mimi ni last born na niko vizuri tu wa kulaumiwa hapo ni nyie wazazi kwani hayo magame kayaokota si mmempa wenyewe jamani.
mlee mtoto kwa njia nzuri bwana wala hataicha hadi atakapokuwa mzee

Point!
Hata mimi ni last born lakini sikuwahi kulaumiwa kwa u-last born wangu. Ila kuna katabia ambako ninako na sijui ni kwa nini! Napenda sana kuchezea nyonyo!
 
Mimi ni last born ndugu na ndiyo mtoto wa kwanza katika familiya kuaza life mapema na ninajua nini ninachokifanya,malezi yako kwa mtoto wako yanalete impact hiyo

last born na hapo hapo mtoto wa kwanza? sijakuelewa Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…