Jamani housegal wangu.........

asanteni kwa ushauri nimejitahidi kumshauri kwa kutumi ushauri mlionipa, kiukweli imesaidia kiasi ameelewa na amepunguza kulia
 
Wanaume sijui roho zao zikoje!wana roho ngumu hawa viumbe wala hawa hisi vibaya kumfanyie msichana hivi, mwambie avute subra yatakwisha na atasahau,huyo bwana nae atapata wakumsugua roho kuliko alivyo mfanyia mwenzie.
 
Kuweni naye karibu mkimwambia hiyo ni kawaida, atazoea. Nyumbani awaambie wamebadili tarehe mpaka siku ingine itayopangwa.
Jamaa alitumia lugha ya kuoa, kambpitia sasa kamtosa. Mpe pole na mwambie huu ndo ulimwengu na hawa ndo binadamu.
 

Wasiwasi wangu i kuwa yawezekana binti alimhonga kijana tunda na baada ya kijana kulitafuna bila hata ya huruma na hakulipenda au ndizo mbinu zake.........................za kutafunatafuna matunda ya walalahoi kwa mkopo usiolipika basi kachanja mbunga na hilo jingine ni kisingizio tu...........................alimwahidi vipi atamchumbia wakati hata hajapata baraka za wazee............mimi hawa vijana ninawafahamu kwa utapeli wao.................kwanza kampime mtoto wa watu kama hajaunganishwa kwenye mtandao wa wanavirusi.................pili pima kama hana uja wepesi.......................lol
 
jaribu kumtia ila yule aliekua anataka kumuoa ili amuene kua alikua si wa maana na hafai hata kidogo na mungu amemuwezesha kumnusuru na ndoa hiyo!
 
Sasa siawaambie ukweli kama ulivyo wazee wake. Na wewe hata kumshauri aseme kweli huwezi? unanshangaza sana!

Au kisha bebeshwa mzigo? semeni ukweli! maana kama ni posa tu kuvunjwa, inasikitisha lakini si kihivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…