Jamani ID zetu zinaficha mengi, khaa!

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Jamani nahisi wife naye yuko JF lakini hatujuani! Halafu hakuna anayeongeleaga kuhusu JF tukiwa pamoja, so hakuna anayejua kama mwenzie yuko humu au la. Mi na wife tukishaingia home ni family time, hakuna cha kugusa PC wala kuhamishia ofisi nyumbani, labda kuwe na kazi ya ofisi ambayo ni so urgent.

Kasheshe ni pale tunapokuwa tunapiga story za kawaida ndo nachoka! Unakuta mapwenti mengi tu ni ya humu humu JF, tena mengine nili-comment mimi mwenyewe au mengine alicomment mwanamke (sa sijui ni yeye!). Kwahiyo najikuta niko ktk dilemma fulani hivi yaani we acha tu.......

Haya kwa ofisi nako kuna vituko vyake. Kuna jamaa 3 tunashare ofisi. Nao pia hatujuani kuhusu uanachama wetu JF. Kichekesho ni kwenye story sasa wakati wa lunch. Unashangaa mtu anaongelea pwenti ambayo umeimaliza kupost muda huo huo unafunga pc. Sasa unajiuliza hivi huyu ananijua au? basi sometimes huwa nabaki naguna tu mmh mmh manake dah .......eti sipendi tu kujulikana na marafiki wa karibu (workmates, roommates etc including mai-waifu wangu) kuwa niko JF

Hivi na wewe hii hali imeishakutokea? hebu tupe uzoefu wako basi..... au nishauri kuhusu hii hali yangu!
 
duh! mito mimi niko sitak mtu anijue kabisa kama niko jf.
na nashukuru sana jina langu ni gumu so watu hawaliwez na mii mwenyewe sijisemi kabisaa. Miye hata nikimuona mtu anakuja karibu yangu nafunga pc mapema pasi hata kuzima wallah manake na utumbo wangu wa humu lol! huyo mume angezimika jamani asingeamni busara zote nikiwa naye kumbe nsikojulikana niko na pumba kiasi hiki.
 
Last edited by a moderator:
mito dah bora wewe
mimi chichemi lol
 
Last edited by a moderator:
napita tuu kabla ya kwenda kulala. hongera gfsonwin kwa kufikisha rep 13,000
 
Last edited by a moderator:

Ebwana jf raaaa usinijue nisikujue, hili siyo soko la sura bhana.
 
nahisi kama nimetishika.mimi mtu akini pm,na jina langu kamili nalitaja.sasa ina maana nianze kulificha jina langu au vipi?
 
I don't share my laptop either at home or at work.....kwahiyo sina hofu. Nyumbani wanajua kama mimi nacheck JF and they real don't care coz they don't check in.
 
I don't share my laptop either at home or at work.....kwahiyo sina hofu. Nyumbani wanajua kama mimi nacheck JF and they real don't care coz they don't check in.

that mean...uko very safe
 

ignorance is a bliss....
 
Binafs imewah kunitokea,baada ya mabom ya gongo la mboto,kuna siku wahindi walikuwa na sherehe yao kukawa na milipuko,sasa hapa jf watu wakawa wanauliza jamani eee mnasikia huko,kila mtu alisema lake,kuna mmoja akasema mimi nipo kinondoni naskia,aaah,kwakua nami naish kinondon nikamuuliza upo kinondon ipi/.akasema mosko,uh nikamwambia ipi akaelekeza tena,nikamwambia isije ikawa tupo nyumba moja,,,,,katika kuelekeza tukajikuta tunakaa nyumba moja,asbuhi tukawa tunacheka ndo hadi leo,ingawa hatupo nyumba moja ila akiwa hapa najua:israel:
 
wengine hatuna la kuficha maana tunatumia majina yetu halisi, watu wangu wa karibu wapo humu na wanajua me ni member tunapishana tu humu na hakuna shida yeyote na huwa na comment kwenye post zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…