Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Sasa hivi huku mtaani matumbo ya wateule walioko kwenye nafasi ya ngazi ya Wilaya, yanapata moto kila siku. Wanasubiri kwa hamu ili wajue mbivu na mbichi. Hawana utulivu wa mwili na nafsi hasa wale ambao wanahisi nafasi ya kuridishwa ni finyu kwao.
Kwa upande mwingine, wale walio nje ya ulingo wanapiga jaramba, wakivizia kama fisi, ili kuona kama kocha atawapa fursa ya kuingia ulingoni wakati wowote kuanzia sasa.
Naomba kuwasilisha.
NB: Mimi si miongoni mwao; wanaovizia kama fisi au wale wenye matumbo moto.
sikuhizi zile taarifa zilizokua zikivuja sijui wametumia mbinu gani kuziba.Sasa hivi huku mtaani matumbo ya wateule walioko kwenye nafasi ya ngazi ya Wilaya, yanapata moto kila siku. Wanasubiri kwa hamu ili wajue mbivu na mbichi. Hawana utulivu wa mwili na nafsi hasa wale ambao wanahisi nafasi ya kurudishwa ni finyu kwao.
Kwa upande mwingine, wale walio nje ya ulingo wanapiga jaramba, wakivizia kama fisi, ili kuona kama kocha atawapa fursa ya kuingia ulingoni wakati wowote kuanzia sasa.....
Naomba kuwasilisha.
NB: Mimi si miongoni mwao; wanaovizia kama fisi au wale wenye matumbo moto. Mimi mpenzi mtazamaji..
Ila we jamaa duu! Eti "UVCCM mnaenda kulima" 😊😊😊Wahusika watakuwa wameshakununia tayariWanaowaza ni waliokuwa uvccm na chama wakapewa UDC!
Wakurugenzi wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya walioteuliwa wakiwa na miaka pungufu au 45 waliingizwa kwenye mkataba wa kudumu. Watapoteza VXR tu, watarudishwa utumishi au tamisemi au wizara yoyote kwa taaluma zao wanaenda kutumia pick up!
Serikalini patam sana, upate uteuzi ukiwa Mtumishi wa serikali hadi raha.
Wale makanali watarudishwa kikosini, walimu wanarudi kwa ras, usalama wanarudi mikoani na makao makuu, Nk.
Uvccm mnaenda kulima.
Kumbe na Paskali atakuwemo? Basi hongera kwake kama ni kweliWafuatao watakuwepo kwenye orodha hiyo:-
1-Paskali Mayalla.
2-........................