sheria ya kuish na mtu yyte iko hivi
1) muheshimu hata kama ni mdogo kwa nafasi yake
2) usimbague wala kunyanyasa, wala kumdharau yyte yule
3) tenda wema mara nyingi kuliko utendewavyo wewe.
4) usisubiri shukurani kwa wema wako wala usingojee hisani kwa jema lolote
5) fanya kila jambo kwa mtu pasi unafiki wowote ule kama hutaki sema sitak na kama ndiyo sema ndiyo
6)usiwe mwepesi wa kusema wala kulalamika, bali mwepesi wa kusikiliza.
7) siyo kila unachoisikiliza kiusemeshe moyo, hapa utakufa kwa presha na sukari
8)usitake mtu akujue ulivyo asijue undani wako yaani uwe msiri na mambo yako.
9) tambua kuwa siyo wote wanaokupenda, so usilaumu unapoonyeshwa kutokukubalika kwenye nafsi za watu wengine.
10) kamwe usikatishwe tamaa na matendo, maneno ama mitazamo ya watu.
11) fanya mara nyingi uwezavyo kile moyo wako upendacho usiulazimishe moyo.
12)shirikiana na wenzio katika mambo yote ya kaijamii.
13) kamwe usitie fitina kwa jambo la heri au la shari
Kubwa kuliko yote sali sana ili uongezewe hekima ya kuisha na watu na pia upendo kwako uwe ni silaha yako.