Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
NIPENDE HIVI NILIVYO
nipende hivi nilivyo sinambie nibadili
ili niwe utakavyo,nikuridhi yako hali
penda nywele nilonazo,kama nimefunga shungi
sinambie nende nazo,saluni kupaka rangi.
mama kocho kanizaa,ndizo nywele nilonazo
hizi sitii chokaa,ondoa hayo mawazo
na rangi nilozaliwa,nyeusi siibadili
madawa kujichubuwa,mambo hayo sikubali
kifua changu kisawa,mola kaniumba kike
sendi kabisa kutiwa,ya feki nikabandike
midomo yangu kamili,imetulia mororo
kwanini niibadili,sioni yake kasoro
kama tumbo huliridhi,bwana njia iongoze
usinitie maradhi,ati tumbo nipunguze?
niengeze makaliyo,nitie palastiki
yananini nilonayo?hata nikatie feki?
aliniumba muweza,kwa vile yeye ajua
umbo linonipendeza,siendi kujiumbua
mola wangu yakahara,kasema kwenye kitabu
kaniumba umbo bora,kwanini nijiharibu
kama unataka niwe,ndotoni unavyoota
unipendae si mie endelea kutafuta
kama kazi yarabana,kwako wimbo wa marimba
mimi mbona sijaona ,wakwako ulomuumba
kasoro hwishi kutoa,mara lile mara hili
na wewe zimekujaa,hako kiumbe kamili
sura wapenda ya rashida, inakutia wazimu
makalio ya tilda na umbo la mariamu.
wacha wako ubinafsi,kutaka kujiridhisha
kwangu hapana nafasi,nilivyo nimejitosha
na kina dada wenzangu,nyote ninakuonyeni
kaa ushukuru mungu,maumbo alokupeni
hakuna haswaaa kiliko,alokikosea mungu
katika fikira zako akitengeza mzungu?
upungufu wa akili,uchache wa kufikiri
ni haswa ipi shughuli,ilomshinda kahari
acha kujikata kata,kwengine kujiengeza
kujibandika matuta,na kwengine kupunguza,
jishauwe na maringo,ulivyo unapendeza
jua apendae chongo,huapa kuwa kengeza
nipende hivi nilivyo sinambie nibadili
ili niwe utakavyo,nikuridhi yako hali
penda nywele nilonazo,kama nimefunga shungi
sinambie nende nazo,saluni kupaka rangi.
mama kocho kanizaa,ndizo nywele nilonazo
hizi sitii chokaa,ondoa hayo mawazo
na rangi nilozaliwa,nyeusi siibadili
madawa kujichubuwa,mambo hayo sikubali
kifua changu kisawa,mola kaniumba kike
sendi kabisa kutiwa,ya feki nikabandike
midomo yangu kamili,imetulia mororo
kwanini niibadili,sioni yake kasoro
kama tumbo huliridhi,bwana njia iongoze
usinitie maradhi,ati tumbo nipunguze?
niengeze makaliyo,nitie palastiki
yananini nilonayo?hata nikatie feki?
aliniumba muweza,kwa vile yeye ajua
umbo linonipendeza,siendi kujiumbua
mola wangu yakahara,kasema kwenye kitabu
kaniumba umbo bora,kwanini nijiharibu
kama unataka niwe,ndotoni unavyoota
unipendae si mie endelea kutafuta
kama kazi yarabana,kwako wimbo wa marimba
mimi mbona sijaona ,wakwako ulomuumba
kasoro hwishi kutoa,mara lile mara hili
na wewe zimekujaa,hako kiumbe kamili
sura wapenda ya rashida, inakutia wazimu
makalio ya tilda na umbo la mariamu.
wacha wako ubinafsi,kutaka kujiridhisha
kwangu hapana nafasi,nilivyo nimejitosha
na kina dada wenzangu,nyote ninakuonyeni
kaa ushukuru mungu,maumbo alokupeni
hakuna haswaaa kiliko,alokikosea mungu
katika fikira zako akitengeza mzungu?
upungufu wa akili,uchache wa kufikiri
ni haswa ipi shughuli,ilomshinda kahari
acha kujikata kata,kwengine kujiengeza
kujibandika matuta,na kwengine kupunguza,
jishauwe na maringo,ulivyo unapendeza
jua apendae chongo,huapa kuwa kengeza