Jamani " lizzy" utaniua kwa barua yako tamu

Ta Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2011
Posts
3,541
Reaction score
2,187
Mpendwa Ta Kamugisha,

Dhumuni la barua hii ni kutaka kukupa jibu la ombi lako ulilonifikishia takiribani mwezi sasa.Ila kwanza naomba unijulie hali yako ili nipate amani na furaha moyoni kusikia u mzima wa afya.Binafsi si mgonjwa ila upweke unanitawala kwa kutoweza kukutia machoni kila uwapo mawazoni mwangu.

Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.Siwezi kusema nilikupenda ghafla maana ntakua nakudanganya na ninajidanganya pia.Lakini kadiri siku zinavyokimbia ndivyo moyo wangu hua unaongezeka mapigo pale nisikiapo kutoka kwako.Naomba nikwambie ukweli kwamba uliponitamkia mara ya kwamba wanipenda nilishangaa sana maana sikutegemea maneno yale ndani ya kipindi kifupi tu ulichopata kunifahamu.Taratibu nilianza kukuelewa na kuamini kwamba inawezekana maana mapenzi hayapangiliwi.

Baada ya kuchukua muda wangu kukusoma na kukufahamu nimeamua na ningependa kuwa wako mpenzi au hata mkeo huko mbeleni kama nia yako ni thabiti.Nakubali kwasababu nimegundua u mwanaume mzuri mwenye heshima kwa watu na pia mwenye kujiheshimu...mwenye mapenzi na mwenye kujali...mwenye sauti ya kuremba masikio yangu kama kinanda kinachopigwa kwa ujuzi na pia mwenye kujituma.Naahidi ntakua nawe bega kwa bega iwe kwa shida na raha...ntakupenda kwa moyo wangu wote bila kusahau kukuheshimu wewe na mawazo yako.

Natumai barua hii itakuacha mwenye furaha hata kama ilikukuta na huzuni.Naomba utabasamu kwaajili yangu japo sikuoni furaha yako ni yangu pia.Nakupenda sana ewe mfalme wa moyo wangu na ninatumai nitabaki kua malkia na mtawala pekee wa moyo wako.

Wako akupendae Lizzy!

PS
Asante sana kwa nauli ntajitahidi pindi nipatapo nafasi nije mjini kukuona.Natamani sana kuhisi joto lako na mikono yako ikinizunguka.Niyaone macho yako ukiniambia unanipenda pia kuninong‘oneza yaliyo moyoni mwako.ALAFU JIANDAE KULA CHAKULA KIZURI NTAKAPOKUJA...NDIZI UZIPENDAZO NTAKUJA NAZO MWENYEWE.
Kwaheri kwa sasa!

"Raha ya barua iwe tamu kama hii"
 
Kama ni Lizzy mwingine kila lakheri mkuu ..

Kama ni Lizzy aka Lizzy Luu aka mama mchungaji aka hunny bunny ......... nakuambia acha kujifagilia.
 
Wivu sasa, hautaki mwenzio nipendwe au?
 
Mpendwa Ta Kamugisha,

Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.

Wako akupendae Lizzy!

Tupate burudani,tutarejea

A Man Who Can't be Moved - The Script
 
Hivi Miss Kaazi Kweli kweli siku hizi simuoni sana, sijui yuko wapi.
 
Huyo binti ushamaliza kazi. hana ujanja kwako ta kamgisha. Hongera sana kwa kuibua kifaa.
 
Sasa pale atakapokuja mwenyewe na kukana...!
Lakini kama ni kweli basi wastahili hongera kwa kufanikiwa kumzidi kete baba mchungaji!
 
Hahahahahahaha Ta Kamugisha bana. . .asante sana kwakunikumbusha hii kitu. Ngoja nimuombe mtu nauli alafu akishakubali tu namzingua nayo nione reaction. . . Lolzzz

Nwy hongera kwakufanikiwa kutuma pesa ya stamp na bahasha, FINALLY, maana ndivyo vilivyokuwepo kati yako na barua.

Akupendae daima,
Lizzy.
 
Kama ni Lizzy mwingine kila lakheri mkuu ..

Kama ni Lizzy aka Lizzy Luu aka mama mchungaji aka hunny bunny ......... nakuambia acha kujifagilia.
Heheheheh. . . acha afurahi kwa siku mbili tatu bana, kupendwa na kuachwa ni bora kuliko kutokupendwa kabisa.
 
Huyo binti ushamaliza kazi. hana ujanja kwako ta kamgisha. Hongera sana kwa kuibua kifaa.

Kazi gani tena hiyo alomaliza Dubu?

@Amy. . .
Hata sipingi mwaya. Niliandika na kuituma mwenyeweeee.
 
Ha ha ha ha ha, Mh, don't be happy, you might have worn sex, but this is temporary victory.

Mpendwa Ta Kamugisha,

Dhumuni la barua hii ni kutaka kukupa jibu la ombi lako ulilonifikishia takiribani mwezi sasa.Ila kwanza naomba unijulie hali yako ili nipate amani na furaha moyoni kusikia u mzima wa afya.Binafsi si mgonjwa ila upweke unanitawala kwa kutoweza kukutia machoni kila uwapo mawazoni mwangu.

Tangu siku ya kwanza unanisalimia pale tulipokutana mara ya kwanza nilijikuta navutiwa nawe kwa ustaarabu uliouonyesha.Siwezi kusema nilikupenda ghafla maana ntakua nakudanganya na ninajidanganya pia.Lakini kadiri siku zinavyokimbia ndivyo moyo wangu hua unaongezeka mapigo pale nisikiapo kutoka kwako.Naomba nikwambie ukweli kwamba uliponitamkia mara ya kwamba wanipenda nilishangaa sana maana sikutegemea maneno yale ndani ya kipindi kifupi tu ulichopata kunifahamu.Taratibu nilianza kukuelewa na kuamini kwamba inawezekana maana mapenzi hayapangiliwi.

Baada ya kuchukua muda wangu kukusoma na kukufahamu nimeamua na ningependa kuwa wako mpenzi au hata mkeo huko mbeleni kama nia yako ni thabiti.Nakubali kwasababu nimegundua u mwanaume mzuri mwenye heshima kwa watu na pia mwenye kujiheshimu...mwenye mapenzi na mwenye kujali...mwenye sauti ya kuremba masikio yangu kama kinanda kinachopigwa kwa ujuzi na pia mwenye kujituma.Naahidi ntakua nawe bega kwa bega iwe kwa shida na raha...ntakupenda kwa moyo wangu wote bila kusahau kukuheshimu wewe na mawazo yako.

Natumai barua hii itakuacha mwenye furaha hata kama ilikukuta na huzuni.Naomba utabasamu kwaajili yangu japo sikuoni furaha yako ni yangu pia.Nakupenda sana ewe mfalme wa moyo wangu na ninatumai nitabaki kua malkia na mtawala pekee wa moyo wako.

Wako akupendae Lizzy!

PS
Asante sana kwa nauli ntajitahidi pindi nipatapo nafasi nije mjini kukuona.Natamani sana kuhisi joto lako na mikono yako ikinizunguka.Niyaone macho yako ukiniambia unanipenda pia kuninong‘oneza yaliyo moyoni mwako.ALAFU JIANDAE KULA CHAKULA KIZURI NTAKAPOKUJA...NDIZI UZIPENDAZO NTAKUJA NAZO MWENYEWE.
Kwaheri kwa sasa!

"Najua itawauma sana" asiyejua usimwambie maana.
 
Kama ni Lizzy mwingine kila lakheri mkuu ..

Kama ni Lizzy aka Lizzy Luu aka mama mchungaji aka hunny bunny ......... nakuambia acha kujifagilia.

Dah wapi Bishanga ndani Unga Ltd??
Afrodenzi hebu mtafute. Bishanga aje kubadili LOCATION haraka..
 
Back
Top Bottom