Jamani maskini kigoma


First lady,
Kwa siku zote nilizokuwa KG nakwambia nilikua tight vibaya sana. Muda wa kupumua na kulala nao nilikuwa naupata kwa shida. Ukichukulia ukweli kwamba hata kelele za usiku zilikuwa zikinisumbua sana.
Nilisikia kuna eneo linaitwa Gungu lakini sikubahatika kufika huko.
Nilikwenda KG kuona kama nitapata uwezekano wa kufungua kabiashara kangu fulani KG lakini ninasita sana kwa sababu bila ya power, na maji katanisumbua sana. Itanilazimu niingie gharama nyingi zaidi kwa ajili ya kuweka generator na kuweka tanki na kukodi magari ya kunibebea maji kila mara. Gharama zitaongezeka sana na cost of production might be higher too. Bado natafakari niende KG au niache.
Nadhani itanilazimu nipate tena muda wa kurudi kustudy zaidi mazingira ya kuwekeza huko.
Yule mzee wa pale makumbusho bado yupo pale pale na ndiye anayetoa historia ya pale. Na jengo ni lile lile linaloendelea kutumika unaweza kuliona ndani katika picha limejaa nyufa. Hata hivyo kwa sababu wanajenga lingine hatuwezi kushusha lawama zaidi.
 
Hapa ni Kakonko, ni kimji Kikongwe kabisa kiko maeneo ya wilaya ya Kibondo. Nasikia hapa ndio kwao na mh. Askofu mkuu Zakaria Kakobe. Hapa nilishangazwa na vijana hawa ambao walikuwa wakicheza pool saa 6 mchana. Je wanafanya kazi saa ngapi??? watajinasuaje katika huu umasikini unaowanyemelea?



Na hiki ni kituo cha polisi Kakonko. Kiko katika nyumba ambayo iko hoi. Ukiangalia utadhani ni quaters fulani kumbe ni kituo cha polisi.

 
Hapa ni mji unaoitwa Nyakanazi. Ni eneo la wilaya ya Biharamulo lakini wakazi wake wengi ni Waha. Hapa kuna junction ya barabara iendayo Kahama na ile iendayo Biharamulo/Rusumo. Na kwa sababu hiyo pana pilika pilika nyingi kweli. Ni hapa nilipokutana na kikundi cha vijana wengi sana wakiuza asali ambayo wao wanadai ni mbichi. Sielewi tofauti zake; na sielewi iliyopikwa inafananaje na ina athari zipi



Na wakina mama wajasiliamali hawakosekani katika maeneo haya maana mahindi choma yalikuwepo ingawa ni kiangazi.



Wakati tunajinyoosha baada ya safari ndefu tu, mara nikaona kuku na chips pale pembeni ikanilazimu nipasogelee maana nawapenda kuku sana. Wana jf si mnafahamu pale Singida palivyo na kuku wengi? sikuchelea kusogea nipate kuku kwa chips wa Nyakanazi na bei ni sh. 8,000/=.
Mnashangaa? hiyo ndiyo hali jamani. Tena ni mradi anautumikia kijana miaka 13hivi. Sijui ni wake au kuna tajiri yeye ni mpagazi tu! Lakini haka kamtindo ka kutumikisha watoto!?! Hayaaaaa!!!!!!.




Mwisho nikamuona huyu rafiki yangu chini ya hii semi-trela. (Sijui kama mnamuona vizuri?) yuko pale akipata riziki yake. Mara nikakumbuka kwamba aaahh kumbe riziki ipo kama utaitafuta popote bila ugomvi na watu au kuwafisadi wenzio au sio?



Leo naishia hapa. Wana jf mnasemaje????????
 
Du, MU, Tunashukuru kwa habari hii. Nadhani umesema na kutoa evidences za kutosha. Jamani, kama kuna mtu humu JF anafahamiana na akina ZITTO, SELUKAMBA (Mbunge wa CMM, KIGOMA mjini), NSWAZUGWAKO na yule mbunge wa Kibondo (nadhani anaitwa CHIZA) basi wawaassit wafike kuona thread hii....labda wanaweza kuwa na la kusema.

Sishangai kwa nini wabunge wote wa Kigoma na maeneo mengine yenye dhiki kama Lindi nk kukimbilia Dar na kusettle jumla.
 
Yaani mchukia fisadi mie naendelea kukupa thanks kwa kweli habari zinazoambata na picha kwa kweli nazipenda....

Tukipata nane wanaotembea kwenye miji kama wewe tena remote area kama hizi ndio inatupa mwangaza wa kutosha kabisa....naanza fikiri kuiga mfano wako...

Thanks bro.
 

Buswelu uliwahi pia kutembelea thread iliyo na post yangu hii hapa?

Bonyeza hapa = https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/17389-wanaoandamana-kuunga-mkono-hotuba-ya-kikwete-wanauelewa.html
 

Aiiiiiiiiii Sinyolita, mbona majina uliyotaja hapo juu ni very influential katika siasa za nchi chi hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…