Jamani msiwaseme vibaya watumishi wa Mungu

Jamani msiwaseme vibaya watumishi wa Mungu

Joyceline

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Posts
1,010
Reaction score
167
Juzi jpili nilihudhuria kwenye maombi ya ngurumo ya upako na nabii geor davie ambaye aliendesha maombi kwenye ukumbi wa diamond jubilee kwa kweli yesu anatenda miujiza pamoja na kwamba watu watasema mengi lakini nimeshuhudia kwa macho yangu , mimi sitakiwi kujua anatumia nini na anafanya nini bora anataja jina la yesu natakiwa nisikilize maneno.
Mkutano huo ulitangazwa jmosi jioni lakini watu walijaa ile mbaya na hajatangaza kwenye redio wala gazeti tumeambiwa tupashane habari.

Ni hivi nabii geordavie atakuwa anaendesha maombi yake dar kwa muda wa wiki nne kwa sababu lile eneo alilokuwa anatumia kule kisongo arusha mwenyewe kamnyan'ganya na linanunuliwa na mfanya biashara mmoja arusha kwa hiyo wakati eneo lingine linaaandaliwa atakuwa dar kwa muda huo kuna muumini ametoa eneo la ekari 2 ndo liko kwenye matengenezo kwa hiyo kwa muda huo waumini wa dar tutapokea upako live pale makonde maeneo ya mbezi beach.
 
Is this the same nabii that sold photocopies of his hand print in Kisongo? Preaching seems to be a lucrative business venture these days, do churches pay tax? I wonder why these "crusades" do not go to impoverished parts of Tz where the gospel hasn't been as well spread as in the big towns, I'm sure that's how Jesus would've wanted it done. It is written "Many will come in my name..."
 
I wonder why these "crusades" do not go to impoverished parts of Tz where the gospel hasn't been as well spread as in the big towns,

Mkuu hapo unakosea.

Kwenye miji mikubwa ndo kuna kondoo waliopotea wengi zaidi.
 
Wamepotea lakini wamesikia injili, kuna watu huko Tanganyika hawafikiwa na Injili bado.


Wotewote wapo kwenye ubatili, iwe mjini au vitongojini au uswazi, wote tumepungukiwa na utakatifu. Cha msingi sio kumnyooshea kidole 'nabii' kwa nini hajafika huku au kule, mimi na wewe tunaowajibu uleule kama wa 'nabii', lakini bado tupo tumejificha nyuma ya PC. Tujiulize tunafanya nini kuwafikia hao, sio 'nabii' anafanya nini kuwafikia hao.

Shukran
 
sijawahi kuhudhuria mahubiri yake but nilikuwa nakutanaga na msafara wake, kwenye no plate kaziba kaandika "ngurumo ya upako" ana escort kama ya waziri fulani, wengi wanayacfia/wanayapenda mahubiri yake, na wengine wanaongea mengi kuhusu yeye, ndio nyakati za mwisho hizi "manabii" wengi watajitokeza.
 
Wait a minute, mbona heading reads msiwaseme watumishi wa Mungu halafu mleta hoja anasema alihudhuria mahubiri na kutangaza kuwa kutakuwa na upako etc? i dont see the connection, Anyway its good marketing. To be honest I dont believe in any of the so called nabii, mtume etc si kwa sababu mahubiri mabaya no ila ni undeshaji mzima wa hizi ministries kwaninin hamna uwazi kwenye mapato,matumizi, kudelegate mambo mf utakuta mchungai/nabii anamanage kanisa peke yake akisafiri basi mahubiri via tv, all these pose a big question mark to me. I dont know if am wrong but i smell something fishy!
 
2meambiwa tufuate maneno siyo matendo, hutakiwi kujua anafanya nini au anatumia nini ananiombea kwa jina la yesu ninapona, mambo yangu yanafunguka ananisomea mistari ya biblia hayo mengine mimi sina shida nayo kwa sababu namwamini Yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yangu atumie nini , au nini i dont care.
na kama ni swala la kwenda kutangaza injili vijijini huwa anaenda kwani mwaka mzima anakuwaga dar msiongee kwa ushabiki ongeeni vitu mlivyo na uhakika navyo yeye hatutangazii injili nadhani wengi tangu sunday school tunasoma biblia wengiene ni mabigwa wa wokovu lakini hajawahi kuponywa na mambo yake ni mabaya daily ndo mana tukaletewa watu wa kutufungua na vifungo. kama wengine wanavyosema wengi watakuja kwa jina langu mimi kama mkristo natakiwa niangalie kuna mahali unaingia wewe mwenyewe unaona hapa ni usanii mtupu. mchungaji anaombea mtu mwka mzima hajapona yeye akiona imani yako iko chini sana yani umeenda kujaribu hakuombei maana usipopona ndo utamuona muongo, anafanya kazi na watu wenye imani na wasio na imani anawatia moyo wamwamini Mungu ndo watapona mpo hapo?
 
nilisema msiwaseme vibaya sababu najua watu lazima wangecomment vibaya kuhsu haya ninayotaka kuandika.
mimi binafsi naongea habari za huyo mtu siyo kwamba namfanyia promo nina experience nimeanza kuhudhuria maombi yake tangu 2005 mjini arusha mpaka nikaja huku dar kila mara akija nahudhuria , nimeamini na nimebarikiwa kwa hiyo kwa upande wangu sioni tatizo liko wapi but kila m2 ana mtazamo wake.imani yako ndo itakuokoa
 
Nadhani unajua mabaya yake ingawa hujayaweka dhahiri.
Ni hivi nabii geordavie atakuwa anaendesha maombi yake dar kwa muda wa wiki nne kwa sababu lile eneo alilokuwa anatumia kule kisongo arusha mwenyewe kamnyan'ganya na linanunuliwa na mfanya biashara mmoja arusha kwa hiyo wakati eneo lingine linaaandaliwa .

Alipokuwa Arusha alisababisha mama mmoja afariki kwa sababu alishuhudia mambo anayotumia halafu akakimbia, hiyo story ya kuwa amenyang'anywa eneo umeitoa wapi?

atakuwa dar kwa muda huo kuna muumini ametoa eneo la ekari 2 ndo liko kwenye matengenezo kwa hiyo kwa muda huo waumini wa dar tutapokea upako live pale makonde maeneo ya mbezi beach.

Unakumbuka jamaa alietembea uchi kwa TZS 30,000? Nadhani hiyo ni advertise tosha kwa ngurumo. Inawezekana hiyo ilikuwa ni advance team kama rais anapotembelea mahali. Someni alama za nyakati.

lakini nimeshuhudia kwa macho yangu , mimi sitakiwi kujua anatumia nini na anafanya nini bora anataja jina la yesu natakiwa nisikilize maneno.
Mkutano huo ulitangazwa jmosi jioni lakini watu walijaa ile mbaya na hajatangaza kwenye redio wala gazeti tumeambiwa tupashane habari.

Mimi siyo nabii, ila kabla hajaanza hayo mahubiri katika eneo hilo, mtashuhudia mengi
 
Extremism sii nzuri ktk nchi yetu!!

Mara waislamu wanasema dini yao ndo nzuri! mara wakristo wanajiona ndo bora zaidi! Wahindi ndo hivi2!

Kubwa ni kupendana kama wanadamu na kuheshimiana!
 
ametangaza mwenyewe diamond kwamba eneo wamenyan'ganywa na mtu aliyekuwa amewapa na linanunuliwa na mfanyabiashara. siyajui mabaya yake maana mimi ni muumini kama wengine mambo ya mtu sifuatilii.

nadhani story ya yule mama liyekufa hamuijui vizuri ilitiwa chumvi sana na watu mngeijua vizuri wala usingesema hivyo.
 
nadhani story ya yule mama liyekufa hamuijui vizuri ilitiwa chumvi sana na watu mngeijua vizuri wala usingesema hivyo.
Naomba mkuu utuchapie kiduuuchu story ilikuwaje ya yule mama....

...alafu nitafsirrie maana ya neno nabii.....
Ubarikiwe
 
ametangaza mwenyewe diamond kwamba eneo wamenyan'ganywa na mtu aliyekuwa amewapa na linanunuliwa na mfanyabiashara. siyajui mabaya yake maana mimi ni muumini kama wengine mambo ya mtu sifuatilii.

nadhani story ya yule mama liyekufa hamuijui vizuri ilitiwa chumvi sana na watu mngeijua vizuri wala usingesema hivyo.


Dada Joy, twambie basi tuijue vizuri ili tuisemee vyema

Kumbuka in JF we talk openly!
 
2meambiwa tufuate maneno siyo matendo,[/QUOTE]

sawa ila ni ngumu, kumwona mchungaji wangu na kilevi, totos, matumizi mabaya ya sadaka halafu kwenye ibada ananisisitiza nimtolee bwana ni ngumu. Hapa sina pingamizi.

hutakiwi kujua anafanya nini au anatumia nini ananiombea kwa jina la yesu ninapona, mambo yangu yanafunguka

hee, I beg to differ, lazima nijua anatumia nini na anafanya nini, hujasikia wengine huvaa electric devices kuwaangusha watu,mmoja alikamatwa uganda aiport akiwa na hii device, na je kama anatumia witchcraft pia sitakiwi kujua natumia nini simply because kasema jina la Yesu! no way lazima nijua anatumia nini, kumbuka matayo 7:21 sio kila aniitaye bwana,bwana ataingia ufalme wa mbingu ila bali wale wafanyao mapenzi ya Mungu, wengi watakuja watasema bwana kwa jina lako tulihubiri, kwa jina lako tulitoa pepo, tuliponya,tulifanya miujiza lakini atawaambia,nendeni zenu enyi waongo.


yeyyeye hatutangazii injili
Mimi nilidhani kutangaza injili ndio first mission Yesu aliyowatuma watu kufanya, soma matayo 28:19 enendeni ulimwenguni kote mkawafundishe na kuwabatiza kwa jina la baba na mwana na roho mt. na kuwafundisha yote niliyowaamuru.

na injili yotee tunaonyeshwa jinsi yesu alivyohubiri watu waache dhambi, watubu wamrudie Mungu ndipo miujuza na uponyaji ulifuata.

[QUOTE]wengi tangu sunday school tunasoma biblia wengiene ni mabigwa wa wokovu lakini hajawahi kuponywa na mambo yake ni mabaya daily ndo mana tukaletewa watu wa kutufungua na vifungo.
Sawa huko sunday school si tunafundishwa mema na mabaya na si mwanadamu amepewa utashi wa kuchagua mema na mabaya, na kwa kuwa tumeelekezwa huko sunday school hatuna budi kufuata,swala la mtu kukengeuka anafanya huku akijua lipi jema.Kwa hiyo hawa manabii hutupa nguvu ya kupinga utashi tuliopewa wa kuchagua jema au baya kwamba tukiombewa tunachagua jema tu? Suala la mtu kuwa hajawahi kuponywa ni dalili ndio sababu ya kwenda kwa nabii? napenda tu kueleweshwa.


kama wengine wanavyosema wengi watakuja kwa jina langu mimi kama mkristo natakiwa niangalie kuna mahali unaingia wewe mwenyewe unaona hapa ni usanii mtupu. mchungaji anaombea mtu mwka mzima hajapona

Sawa kwa hiyo muda gani utumike kama kipimo, kwamba nisipoponywa within a year nihamie kwa nabii mwingine, au nipofanikiwa mambo yangu ndani ya mwezi nitafute maombi pengine?

anafanya kazi na watu wenye imani na wasio na imani anawatia moyo wamwamini Mungu ndo watapona mpo hapo?
sawa

mwisho nina swali hivi kwenye biblia tunaona kweli Uponyaji ulitokea na miujiza ila kwa ufahamu wangu mdogo nasoma kuwa mara nyingi yesu alipofanya miujiza aliwasihi wale walioponywa wasitangaze kwa watu, napata wazo kuwa Yesu hakutaka ionekane kuwa kazi kubwa ya ukombozi ni miujiza ila kubadili roho za watu, waache dhambi. Nachelea kuamini huu uponyaji wa siku hizi, wahubiri wameelemea kwenye mijuiza yaani mabadiliko ya miili (ikiwemo kufanikiwa kupata visa, magari, utajiri-niliangalia mahubiri fulani mhubiri alisisitiza waliokosa visa waende waombewe, wanaotaka utajiri waombewe nk) badala ya kuhubiri ukombozi wa roho.
Pili, kwa nini hili wimbi la wahubiri wanaofanya miujiza limeongezeka kwa kasi miaka hii? ina maana makanisa yetu huko nyuma hajafanya kazi ipasavyo? Na mijini ndio kwenye watu wenye matatizo sanaaa maana ministry nyingi ziko mjijini.
Nikieleweshwa kwenye hili basi nitaacha udadisi.
 
ametangaza mwenyewe diamond kwamba eneo wamenyan'ganywa na mtu aliyekuwa amewapa na linanunuliwa na mfanyabiashara. siyajui mabaya yake maana mimi ni muumini kama wengine mambo ya mtu sifuatilii.

Kama hivyo ndivyo, iweje mtu ajitolee kwa mambo ya mwenyezi mungu alafu abadili mawazo na kuelekeza kibiashara?

Halafu hapo umeongelea nafsi zaidi ya moja. Unauhakika na unachoandika au ndio nguvu za ngurumo?

nadhani story ya yule mama liyekufa hamuijui vizuri ilitiwa chumvi sana na watu mngeijua vizuri wala usingesema hivyo.

Joy acha kuwa mnafiki, unajua wazi mambo yake ndo maana unasema huyafuatilii. Na je, ni kwanini asitangaze kwenye WAPO redio au redio Tumaini ili awapate waumini zaidi? Anajua anachokwepa.
 
Back
Top Bottom