Jamani msiwaseme vibaya watumishi wa Mungu


Mwisho upi?

Acha kutisha watu! Hata miaka 1300 AD walisema ni wakati wa mwisho leo ni 2009!

Mtu ukushakuwa brain washed na dini you can not think beyond the box!
 
1) tujue tuko katika nyakati za mwisho - nyakati ambazo maasi yameongezeka kwa kiwango cha juu - always - maasi yanapoongezeka, neema ya Mungu inaongezeka

Watu wa dini kwa kujifariji mmmh!
Nyakati za mwisho zilisha sikika enzi hizo hata babu wa babu yako hajazaliwa.
We utatangulia watakuja wengine nao watadanganywa hivyo hivyo kama wewe eti nyakati za mwisho.Wakati wa mwisho ni kufa kwako wewe na kupotea na kurudi mavumbini hapo ndo unakuwa wakati wako wa mwisho acha kuogofya watu wenye mioyo miepesi.Mlidanganya ooh 2000 ndo mwisho wa dunia tunadunda mpaka kesho.
 



.


Kwa hiyo kuna haja ya hospatal , wakati BWANA anaponya.
 



.


Imani yako ndio ikayo kuokoa au kukuangamiza! Nabii? Karnehii iliyo jaa wajanja na vituko vya kila aina kuna na bii kweli? ...Ndio waliwao.
 
Joyceline
Kabla ya 2005 ulikuwa unasali kanisa gani? Je hukuwa na imani huko au nini kilitokea
ukahamia hilo kanisa jipya?

Dini yako ndiyo imani yako,hiki ni kitu cha kukumbuka.
 
.
Hayo mambo ya kudanganyana, kuponya, kufunguliwa! Hayapo kwao.
 
.
Hawa manabii waleo mbona hawawaponyi wenye ukimwi?, mbona hawaombi utajiri wanawakamua waumini wao tu! Toeweni sadaka mtafunguliwa mbona hawajifunguwi wao kwanza?
 



.


Thats right.
 



.


Hakuna mwanzo usio namwisho.
 

Naomba kueleweshwa tumeambiwa kuwa manabii karibu wote waliteremshiwa vitabu na Mmungu sasa huyu Nabii geor davie ameletwa au ameteremshiwa kitabu kipi?
 
Watu wakishindwa kukabiliana na Mazingira ya maisha hukimbilia kwenye imani, mie nabii mie nani. WIZI MTUPU
 
Tusiwaseme vibaya watumishi wa Mungu? kwa vipi? Kuwasema vibaya vipi?
Mi nadhani maisha yao ndiyo yatawasema walivyo na si vibaya watu wakasema na kutoa tahadhali kwa kile wanadhani hakiko sawa katika utumishi wa wajamaa wengine. Vinginevyo tukitaka kusifia tuuuuuuuuuu WATAPOTEA YAMKINI NA WATEULE. Najua wengi hawapendi criticism wakati tunajua hata Yesu halikuwa criticised hakujali. Alikubali kila kitu.
 
kwikwikwikwikwi watz siku hizi tunachanganyikiwa najua maisha yamekuwa magumu.......

Kwanini tuchanganyikiwe? sidhani kama solution ni kuhama hama dini eti kwa vile una shida fulani unataka itatuliwe. Haya maisha magumu hayajaanza leo wala jana!

Kama una dini yako tulia nayo, uwe na imani kwa kila uombalo au unachokiabudu!
 
..nasikia kuna wengine wana kanisa lao linaitwa la Watakatifu waliopo duniani. Inakoelekea kuna mashindano pia ya kutumia vivumishi vya sifa kwenye majina na vyeo vya wahubiri wao. ni lazima kila mmoja awe askofu, nabii, mtume?
 

Mathayo 7:15, 21-23 "Jihadharini na manabii wa uongo watu wanowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali. 21-23, Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu."
 

Wawe na uwazi kwenye mapato na matumizi yao wachekwe? Maana wakifanya hivyo wafuasi wao watagundua kama hawa jamaa nao ni mafisadi tu ambao wanaishi maisha ya hali ya juu kwa michango chungu nzima toka kwa waumini wao na wakati huo huo hawana unabii wowote ule ni wanafiki tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…