JAMANI Mwanafunzi Mwenzenu Naomba Ushauri.

Sweetlicious

Member
Joined
Nov 1, 2013
Posts
70
Reaction score
26
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21, nasoma mwaka wa 3 kwenye chuo kikuu kimoja cha hapa mjini, nafanya shahada ya miaka minne, nimezaliwa na kukulia kwenye familia bora, tumezaliwa wanne na mimi ni wa mwisho, kaka zangu wawili wamezaliwa na Baba kutoka Uingereza, kaka yangu ninayemfuata amezaliwa na baba toka Benin, na mimi Baba yangu ni Myahudi raia wa Israel, wote Mama na ndugu zangu wako nje ya Nchi na Mama anafanya kazi shirika la chakula duniani Nchini Italy, nimebahatika kusoma nje lakini muda mwingi wa makuzi nilikuwa na bibi yangu hapa Tanzania, wakati nikiwa mwaka wa kwanza semester ya pili nilifeli kozi moja amabayo hata sikuitegemea na wenzangu walinishangaa richa ya uwezo wangu mkubwa wa kiakili (Mimi ni mchanganyiko wa myahudi na Mchaga), katika kufeli nililazimika kuirudia nikiwa mwaka wa pili, kwa bahati nzuri nikaiondoa, lakini katika hilo Professor aliekuwa ananisimamia hiyo kozi alianza kunitaka kimapenzi nami kwa juhudi kubwa nilimkatalia, lakini kwa vile nilikuwa najua kuna mahusiano makubwa kwanini nilifeli mwaka wa kwanza na Prof kuanza kunifatilia niliisoma hiyo hali nikajenga mazoea na yeye, mpaka akajua tayari nimeisha ingia kwenye mstari wake, alianza kwa kunipigia sana simu zisizo na idadi tena kwa number tofauti na mpaka leo sijui number yangu aliitolea wapi, alinitaka mara kibao tutoke lakini nilimkatalia mpaka wakati fulani nikamtania kama anataka kutoka na mimi basi labda twende nje ya Nchi, baada ya majuma kadhaa aliniita nikamkuta kwenye ofisi yake ya mjini ambapo alinionyesha bahasha tatu, mbili zikiwa na tiketi mbili za Ndege, moja ikiwa na jina lake na nyingine majina yangu kamili, na bahasha ya tatu ikiwa na fedha ambazo baadae nilizihesabu zilikuwa ni zaidi ya 1.5M maana asubuhi yake nilimwambia kwa utani nina shida ya kifedha, na akaniambia ametimiza matakwa yangu ya kutoka nje ya Nchi, kiufupi nilishindwa kumkatalia nikakubali siku ya siku Alhamisi tulisafiri kwenda kwenye mji mkuu mmoja maarufu hapa Africa, tulifikia hotel ya 5 star, baadae niligundua kwamba alikuwa na mhadhara Jumamosi kwenye chuo fulani maarufu kwenye hio Nchi na Africa, tuliongea sana katika safari hiyo akinieleza matatizo yake hasa ya kifamilia na mkewe (ameoa na ana watoto wawili) akisema yeye ni mtu tajiri lakini hana raha kabisa, wakati tukienda huko niliamua kwamba sitofanya nae mapenzi, tulifika mapema kabla ya asubuhi, tulienda kwenye maduka makubwa akaninunulia vitu vingi, a really smart phone, smart Ipad, nguo nyingi nzuri zikiwamo za ndani akinichagulia mwenyewe, viatu, mikoba, saa, mikufu, pete kila kitu, nahisi kabisa ile shoping iligharimu karibu 5M, tulienda migahawa mizuri sana hata wakati nikihisi nimeshiba sana, siku hiyo nililala peke yangu usiku wa Alhamis, Ijumaa alikuwa busy anaandaa presentation yake ingawa baadae tulienda kupima UKIMWI kwani alihisi mimi namuogopa kwa sababu hiyo kwenye crinic moja kubwa kwenye jiji hilo, na jumamosi alienda kupresent ambapo alirudi akiwa amefurahi sana kwamba amefanya vizuri katika hiyo presentation na watu wamemsifu sana, akaniambia tutoke kwani alikuwa amealikwa na marafiki zake chakula cha usiku baadae tulienda na alinitambulisha kama girlfriend wake kutoka Israel, tulikutana na watu wa Uganda na Kenya mahali hapo nilijifanya sizungumzi kabisa Kiswahili, ila kwa bahati nzuri nina accent ya kiingereza, tulikunywa na kulewa sana, tukarudi hotelini kwetu baadae ambapo kwakweli sikuwa na akili yangu nilifanya nae mapenzi usiku wote, tulirudi Nchini nikiwa mtu tofauti mwenye mawazo kidogo lakini sikuwa na wasiwasi.... nimekutana nae mara kadhaa hapa mjini na nje ya Nchi mara kadhaa tena, ni mtu msomi mwenye mialiko mingi ya kimataifa kila akiwa na safari ya mbali lazima twende wote mara mbili tumeenda wote Ulaya, na sasa ameniambia anataka twende tena huko mbali, amenibadilishia gari langu.... na nimerekebisha kidogo moja ya Nyumba za familia yangu ambayo ndio ninayoishi na sehemu nyingine nimerent, na bado ananipa kiwango kikubwa cha fedha nimenunua uwanja, nimefungulia biashara zangu tatu amabazo hazijui....kinachonisumbua yeye ni mume wa mtu mwingine, bababa wa watoto wake, nami ni mwanafunzi binti mdogo, natamani kuwa na msomi wa kariba yangu... nilikuwa na mtu mwanafunzi wa Chuo kingine tuliachana kwa sababu alikuwa mkali, mwenye wivu, na mlalamishi... naogopa nikimuacha itakuaje, nikimkatalia kuna hatari akatufundisha tena mwaka wa nne kwani ndie mtaalamu wa fani hiyo kwenye kitivo na anasifika kwa kudaka vichwa hasahasa finals...nimechanganyikiwa naomba ushauri wenu, nina akili zangu timamu, najua kwamba nilishindwa kusimamia maadili yangu vizuri hapo katikati lakini naamini kwamba nilianguka na naweza kusimama, nina uwezo wa kiuchumi wa kujisimamia na kutumia, hata favors zake ni nyogeza tu ya kutumia zaidi natanguliza samahani kwa watakaokerwa ntazingatia ushauri wenu. (imetafasiriwa kutoka kwenye lugha ya Kiingereza kwa msaada wa rafiki)
 
mi nafikir kwa sabab kashakutumia mpaka karib anakuchoka endelea nae tu umalize hiyo koz yako ukimuacha lazima udisco na ukimaliza hiyo koz yako nenda kanisan kalale week ukitubu hiyo dhambi yako. over!
Noted!
 
mi nafikir kwa sabab kashakutumia mpaka karib anakuchoka endelea nae tu umalize hiyo koz yako ukimuacha lazima udisco na ukimaliza hiyo koz yako nenda kanisan kalale week ukitubu hiyo dhambi yako. over!
Mamaaaaaa! OMG!
 
Endelea nae tu mbona ushado naye mara kibao. We malizia shule kwanza ndo ufuate ustarabu wako. Ukirukaruka sasa na tayari ushaingia mtegoni ndo utazidi kuumia.
 
yani km nilikuwa nasoma story jamani.Hivi wewe umekula vyake weeee leo ndo unaomba ushauri.kwenye story yako ulivyokuwa nje ulisema ulijifanya hujui kiswahili halafu mwisho wa story unadai imetafsiriwa jamani mhhh!!!"
 
yani km nilikuwa nasoma story jamani.Hivi wewe umekula vyake weeee leo ndo unaomba ushauri.kwenye story yako ulivyokuwa nje ulisema ulijifanya hujui kiswahili halafu mwisho wa story unadai imetafsiriwa jamani mhhh!!!"
Mwenzio akil imerud saiv hali hii haiwezi kuendelea, naweza swahili kuongea pia lakini sio swahili mufti sana zaidi ntazingtia ushuri wako mtoto wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…