Jamani naomba msaada wenu, mtoto wangu ana miaka miwili na miezi saba, katika siku za hivi karibuni kuna dalili naiona kama anapata kigugumizi wakati anaongea kitu ambacho hakikuwepo hapo kabla. Wakati mwingine anashindwa kutamka neno anaamua kunyamaza au kama akiongea basi anajitahidi kuongea kwa kuweka mkono mdomoni.
Jamani hii ni shida gani? Msaada please.
Kama ni kigugumizi hakuwa nacho mpaka hali hii ilivyoanza karibuni