Jamani naombeni ushauri.

Jamani naombeni ushauri.

Rafia

Member
Joined
Nov 20, 2013
Posts
26
Reaction score
2
kwanza napenda kuwasalimu.na poleni kwa majukumu.Nimekuja hapa jukwaan kuomba msaada wa mawazo.Mimi ni mwajiriwa wa serikali(mwl) kipato changu hakikidhi mahitaji yangu ya kila cku.napenda sn kijishughulisha lkn bado cjapata pa kujishikiza walau niingize ht 1000 kwa cku ktk muda ule ninapotoka kazni jion.naomba ushaur wenu.nipo MOSHI.
 
Siku hizi walimu wote wanavyama vyao vya kuweka na kukopa (saccos), ni vyema ukafanya utaratibu wa kujiunga na vyama hivyo, maana maisha ya ajira za serikali kwa Tanzania bila mikopo huwezi kuwa na maendeleo unayoyahitaji!
 
Kama unapata muda wakati wa jioni kwa nini usianzishe tuition yako kwa masomo unayofundisha na itakua rahisi kwa wewe kuitangaza kwa wanafunzi wako 200 kwa siku mara wanafunzi 10 tayari 2000 kwa siku.
 
asante mkuu kwa ushaur wako bt maeneo nilipo hakuna mwamko wa elimu kivile so tuition inakuwa ngumu kdg.
 
jaribu tuition kama ulivyoshauriwa ila uwe mvumilivu sana. ata ukiwa na wanafunzi wawili miezi sita usiache. tuition ishu nikupata jina kwanza.
 
asante mkuu kwa ushaur wako bt maeneo nilipo hakuna mwamko wa elimu kivile so tuition inakuwa ngumu kdg.

moshi wapi hamna mwamko wa elimu? acha woga anza tuition. tafuta wanafunzi wawili uanze kuwafundisha bure.
 
moshi hamna mwamko wa elimu?
au ni mbatakero kule umasaini?
_sema upo moshi sehemu gani maana kuna maeneo moshi unaweza kukodi shamba ukalima na ukavuna tu
 
asante mkuu kwa ushaur wako bt maeneo nilipo hakuna mwamko wa elimu kivile so tuition inakuwa ngumu kdg.

ni sawa Rafia huenda maeneo uliyopo kukawa kuna mwamko wa elimu lakini hakuna mwamko wa kuwapeleka watoto masomo ya ziada kwa sababu tofauti tofauti. Lakini unayo nafasi ya kuangalia nini ufanye ili uweze kujiongezea kipato coz inakuwa ngumu kidogo kukushauri na sijajua wewe ni mwalimu wa primary au secondary. kama ni primary unaweza kutengeneza vijitabu vidogo vidogo vyenye kurasa kama 20 hivi vya wanafunzi wa std 1 hadi std 3 vya kwa masomo kama kingereza,kiswahili,sayansi,hesabu n.k na kuuza kwa bei ya 3,000 kwa kitabu au kama ni secondary unaweza kuandaa notes nzuri kisha ukauza kwa wanafunzi masomo kama history,geography,commerce,chemistry e.t.c.
vile vile unaweza kuwe unatengeneza some bites nzuri kama sambusa,chapati,bagia, kisha ukawa unawauzia walimu wenzako hapo ofisini
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom