Jamani ndani hodini, hamjambo afya zenu
Najiingiza kundini, naomba karibu zenu
Nijipenyeze pembeni, niweze kuwa wakwenu
Mzizi wa Mbuyu laivu, jamiini naingia
Wakuu wa tafakuri, nipeni japo nafasi
Njimwaye na kufikiri, Bongo nilitie chansi
Nizunguke ka tairi, mtandao si nanasi
Mzizi wa Mbuyu laivu, jamiini naingia
Asante mkurugenzi Babu Ataka Kusema, tuko pamoja. Ila naona wengine ushairi umewapiga kachenga, "but I thank you all in this house" nimefurahi sana kuwa ndugu yenu naamini sitawaangusha.
Umefanya vema kumkaribisha,lakini unaposema ajisikie yuko nyumbani, napaka wasiwasi kwa sababu hatujui nyumbani kwake kukoje. Je kama nyumbani kwake anapigwa ina maana na hapa atapigwa?
Asanteni tena, ila wengine wanapenda utani sana humu ndani kama huyu Malila, sipigwi nyumbani chifu, naitwa baba. Mambo jambo, na mzee wa "ka-chawa kanakozunguka nimewapata.