Jamani, nimeokota mapesa!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
Heshima zenu Wakuu! Nawaletea habari ya kweli, kweli kabisa, maana mimi nauchukia uongo kama ukoma! Nimeokota mapesa. Sasa usiniulize ni dola ngapi, usije ukashawishika kunifuata uninyang’anye! Wewe jua tu nimeokota mapesa kama wana wa Israeli walivyookota “mana” jangwani. Mimi nafanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato. Hata hivyo, pamoja na kufanya kazi ninamtegemea Mungu kila wakati, kwakuwa najua unaweza kufanya biashara usipate wateja/pesa. Unaweza kuajiriwa ukafukuzwa kazi. Unaweza kupata pesa zikaibiwa zote! Hivyo ni muhimu kumtegemea Mungu. Kwa kufanya hivyo nimeona Mungu akinifanikisha na kunitendea miujiza mingi.

Haya, turudi kwenye mada. Ilikuwa hivi: Kuna watu watatu walikuja ofisini kwangu wiki iliyopita, kwa wakati tofauti na siku tofauti. Wote ninawafahamu na huwa ninawasiliana nao. Niliwahudumia wakaondoka. Jana mchana, niliingia ofisini kwangu, nikachungulia chini ya viti vya wageni. Kwa mshangao mkubwa nikaona mapesa! Mimi ni mwaminifu sana kwa habari ya pesa. Nikija dukani kwako ukinizidishia chenji nakurudishia. Nikasema moyoni mwangu haya mapesa nadhani ni wale jamaa waliokuja ofisini kwangu wameyadondosha. Siwezi kuyatumia. Nikawapigia simu na kuwauliza kama waliona upungufu wa pesa kwenye mifuko yao baada ya kuondoka. Wote wakakataa na kunipa kibali cha kuyatumia hayo mapesa.

Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi. Tangu nimwamini Yesu, nimeona miujiza mingi ya kupita kawaida. Hata huo ni muujiza. Nilikuwa na shida ya pesa, nikamuomba Mungu, amenipa mapesaaa! Stay blessed!
 
tatizo CCM ndugu yangu, hawa ndio wanatuacha tunakua na ndoto
 
Ni kweli ukiwa na bwana kila kitu ni raha sana nilikiwa nateseka na mengi ila naona mwanga
 
Today is Money Day, let the Mighty God be praised just because of the miracle you have encountered
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…