Jamani, nimeokota mapesa!

Hadharani ni wapi? This is a public forum. Hapa ni hadharani zaidi ya madhabahuni, Mkuu.
basi mpe sifa na utukufu kwa neema alizokujalia badala ya kujisifu kibinafsi ya kwamba u mwema
 


Heshima zenu Wakuu! Nawaletea habari ya kweli, kweli kabisa, maana mimi nauchukia uongo kama ukoma! Nimeokota mapesa. Sasa usiniulize ni dola ngapi, usije ukashawishika kunifuata uninyang’anye! Wewe jua tu nimeokota mapesa kama wana wa Israeli walivyookota “mana” jangwani. Mimi nafanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato. Hata hivyo, pamoja na kufanya kazi ninamtegemea Mungu kila wakati, kwakuwa najua unaweza kufanya biashara usipate wateja/pesa. Unaweza kuajiriwa ukafukuzwa kazi. Unaweza kupata pesa zikaibiwa zote! Hivyo ni muhimu kumtegemea Mungu. Kwa kufanya hivyo nimeona Mungu akinifanikisha na kunitendea miujiza mingi.

Haya, turudi kwenye mada. Ilikuwa hivi: Kuna watu watatu walikuja ofisini kwangu wiki iliyopita, kwa wakati tofauti na siku tofauti. Wote ninawafahamu na huwa ninawasiliana nao. Niliwahudumia wakaondoka. Jana mchana, niliingia ofisini kwangu, nikachungulia chini ya viti vya wageni. Kwa mshangao mkubwa nikaona mapesa! Mimi ni mwaminifu sana kwa habari ya pesa. Nikija dukani kwako ukinizidishia chenji nakurudishia. Nikasema moyoni mwangu haya mapesa nadhani ni wale jamaa waliokuja ofisini kwangu wameyadondosha. Siwezi kuyatumia. Nikawapigia simu na kuwauliza kama waliona upungufu wa pesa kwenye mifuko yao baada ya kuondoka. Wote wakakataa na kunipa kibali cha kuyatumia hayo mapesa.

Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi. Tangu nimwamini Yesu, nimeona miujiza mingi ya kupita kawaida. Hata huo ni muujiza. Nilikuwa na shida ya pesa, nikamuomba Mungu, amenipa mapesaaa! Stay blessed!

"Anchored in truths sublime, virtues noble, equity unwavering, purity radiant, beauty transcendent, and all that merits exaltation."
— Embodying the quintessence of Philippians 4:8

 
Mkuu, usichanganye masomo. Kujisifu na kujitambulisha ni vitu viwili tofauti. Mimi hapo ni kama nimeandika tu CV. Nimejitambulisha tabia yangu na mwenendo wangu ulivyo. Halafu soma Maandiko haya umhukumu Mtume Paulo aliyejisifu:

2 Kor 11:23​

Hata mimi ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.

2 Kor 11:16​

Nasema tena, mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; ili mimi nami nipate kujisifu ngaa kidogo.
 
Anchored in truths sublime, virtues noble, equity unwavering, purity radiant, beauty transcendent, and all that merits exaltation."
Tlaatlaah, there's a clear distinction between merely describing one's character and engaging in boastful behavior. When I say that I'm honest, I detest lies, and I work hard, I'm simply sharing the truth about who I am. I am anchored in truths sublime, virtues noble, equity unwavering, purity radiant, beauty transcendent, and all that merits exaltation. That is an honest self-assessment based on my personal values and behaviors.

In contrast, boasting usually involves exaggerating one's qualities or achievements to seek external validation or admiration. It often has an element of self-aggrandizement, where the focus is more on how impressive one appears rather than on accurately portraying one's character.

So, while you might interpret my honest self-description as boasting, my intention is simply to communicate my true values and lifestyle, not to inflate my image for praise. Only God deserves praise.
 
relax,
plz my lady
 
Mungu akubariki sana mpendwa wangu,

Kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Aimen
 
Maelezo yako yanatia mashaka, bora usingesema chini ya kiti.
 
Pumbavu wewe unanifundishannini kuhusu kuokoka, mwenyewe nliona humu unawatukana watu matusi ya nguoni, fala nini danga wewe.
Mkuu, tujiepushe na maneno ya kubomoa. Katika Waefeso 4:29 tunaambiwa neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwetu, bali lililo jema ili liwajenge wanaosikia.
Hatari zaidi ni kwamba watu wanaotukana hawataurithi ufalme wa Mungu: Katika 1 Kor 6:9-10 imeandikwa hivi: "Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi(1 Kor 6:9-10).
 

Binafsi siamini sana kwenye kuokota pesa kama bahati japo yaweza kuwa bahati. Kunauwezekano kuna mtu analia huko kwa kushindwa kufunga mzigo wake wa biashara au pengine kulipa ada nk nk
Ungesema umepata dili la pesa ndefu ningekuelewa....
 
Sas hapo Mungu na mwanae wa pekee wameingiaje?
mbona mnawasingizia vitu vingine
 
Na yule aliyepoteza Hela naye kasema "oooh my god nimefanya Nini hiki 😉😉😉

Maisha sio Fair anyway hongera
Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi
 
Na yule aliyepoteza Hela naye kasema "oooh my god nimefanya Nini hiki 😉😉😉

Maisha sio Fair anyway hongera
Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi
 
Na yule aliyepoteza Hela naye kasema "oooh my god nimefanya Nini hiki 😉😉😉

Maisha sio Fair anyway hongera
Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi
 
Aisee, hebu niazime laki tano tu!
 
Jamani,jamani,jamani tafadhalini mkamateni huyu jamaa,mfungeni na kamba kabisa jamani,anapoelekea sio kuzuri kabisa jamani
 
Pumbavu wewe unanifundishannini kuhusu kuokoka, mwenyewe nliona humu unawatukana watu matusi ya nguoni, fala nini danga wewe.
Huyo ni shetani mwambie akuachie nenda kanisani mie nikabla sijaenda kanisani Mwambie Mungu akusamehe maana hunijui mimi ninani naishije na usipende kuhukumu mtu maana wewe ni mwanadamu tu huna hadhi ya kuhukumu sio jukumu lako hujaambia uokoke.

Nenda kanisani
 
Kwendaaa huko. Unatukana watu matusi ya nguoni halaf unanifundisha kwenda kanisani, bladyfool. Wewe ndio ukaokoke kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…