Jamani nina million 2 nataka kuanzisha biashara, nishaurini

Jamani nina million 2 nataka kuanzisha biashara, nishaurini

meckbash

Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
93
Reaction score
30
Ndugu zangu,

Mimi nikijana nina kiasi hicho cha pesa nataka anzisha biashara lakini nashindwa jua ipi itanifaa kulingana na mtaji huo lakini pesa ya kula na kulala ninayo mtaji tu ndio mil 2.
 
fungua grocery mkuu,, Watanzania wengi wana stress na maisha magumu,,wameamua kujilipua kwa kunywa viroba
 
mkuu mi nakushauri jikite zaidi katika njia iliyokuwezesha kuipata hii milioni 2......................
 
Kama ameiba je?

hahaaa au kaokota looh.

Kwa mtoa mada:
Sina uzoefu sanaaa na mabo ya biashara ila uzalishaji upo wa aina nyingi. Mie huwa naamini kwenye kidogo na kukua kuwa kikubwa. Mahali unapoishi angalia changamoto zinazoikabili hilo eneo, zishuhulikie utoze pesa. Mfano waweza anzisha kigenge kwa maana unaenda nunua vitu alfajiri kwa bei chee unakuja kuuza kwa bei juu kidogo ila iwapo hakuna vigenge karibu, na hii uifanye mwenyewe. Pia waweza amua kwenda nunua vitu kariakoo kwenye maduka ya jumla na kuja kuuza mtaani kwenu maana hapo uwe na fremu ambapo fremi za mitaani naamini bei zake si sawa na bei za kariakoo hivo utapata faida.
La kama aneo unaloishi lina wakazi wengi anzisha biashara ya chips na vitu kama urojo vitafunwa tafunwa vya jioni ambavyo watu watakaa kula .
Chambua hayo ngoja na wengine waje.
Ajuza bibi Kasie.
 
tuwasiliane nikuuzie pub yangu! Mimi Kwa sasa biashara zangu ni za kusafiri sana nakosa usimamizi
 
pub yako iko maeneo gani??
hebu shar na eturns zako kwa mwezi
 
Fuga Nguruwe, Anza Nao Ndama 20 Kwa 800,000
 
Back
Top Bottom