Mimi nikijana nina kiasi hicho cha pesa nataka anzisha biashara lakini nashindwa jua ipi itanifaa kulingana na mtaji huo lakini pesa ya kula na kulala ninayo mtaji tu ndio mil 2.
Kwa mtoa mada:
Sina uzoefu sanaaa na mabo ya biashara ila uzalishaji upo wa aina nyingi. Mie huwa naamini kwenye kidogo na kukua kuwa kikubwa. Mahali unapoishi angalia changamoto zinazoikabili hilo eneo, zishuhulikie utoze pesa. Mfano waweza anzisha kigenge kwa maana unaenda nunua vitu alfajiri kwa bei chee unakuja kuuza kwa bei juu kidogo ila iwapo hakuna vigenge karibu, na hii uifanye mwenyewe. Pia waweza amua kwenda nunua vitu kariakoo kwenye maduka ya jumla na kuja kuuza mtaani kwenu maana hapo uwe na fremu ambapo fremi za mitaani naamini bei zake si sawa na bei za kariakoo hivo utapata faida.
La kama aneo unaloishi lina wakazi wengi anzisha biashara ya chips na vitu kama urojo vitafunwa tafunwa vya jioni ambavyo watu watakaa kula .
Chambua hayo ngoja na wengine waje.
Ajuza bibi Kasie.