Jamani nisaidieni-huyu dada ananipa presha.

Dada Lizzy, naona umetutoa kwenye thread, yaani wewe kwa kusoma tu hiyo stori ya ndugu yetu huyo unakuwa mkali kama wewe ndo umeumizwa?, Nadhani msamehe mshauri nini afanye kuepukana na dhahama iliyomkuta, na achukue hatua gani ili asirudie!
 
Hii pombe mnaisingizia vingi sana...... pombe ndo ilimvulisha chupi? Ndo ilimpa namba za simu? Ndo inatukana?...Wakati ameanza kuzoeana naye na kumkaribisha pombe akijua ana mke home, ni pombe ilimtuma?
Aiseees...ngoja nikuite BABU..hapa tu lakini!!Yani hivi visingizio vya sijui pombe...mara shetani...sijui mwanamke kanirubuni hua vinaboa sana!Angalau mtu awe akubali kwamba yeye ndo aliyesababisha maana hakubakwa wala hakushikiwa mtutu...man up!!
 
Dada Lizzy, naona umetutoa kwenye thread, yaani wewe kwa kusoma tu hiyo stori ya ndugu yetu huyo unakuwa mkali kama wewe ndo umeumizwa?, Nadhani msamehe mshauri nini afanye kuepukana na dhahama iliyomkuta, na achukue hatua gani ili asirudie!
Nimetamani nisikujibu ila naomba kukuuliza....kipi hapo kisichohusika na thread?!
 
Aiseees...ngoja nikuite BABU..hapa tu lakini!!Yani hivi visingizio vya sijui pombe...mara shetani...sijui mwanamke kanirubuni hua vinaboa sana!Angalau mtu awe akubali kwamba yeye ndo aliyesababisha maana hakubakwa wala hakushikiwa mtutu...man up!!
Huna ujanja, mi ni babu yako tu...no matter what na huna ujanja wa kunikimbia...
 
asee pole mkuu...hata mm hii kitu iliwahi kunitokea.....kata kabisa mawasiliano ikibidi hama kabisa maeneo aliyokua anafikia...then badilisha namba ya simu manake inavyoonekana amekupenda kweli mkuu ana ana kama ukichaa hv
 
Walitoka out huku na huku Majoja akajikuta anakagua baada ya kupiga chicha
Kabla hawajaenda kupiga chicha, ni pombe ndo ilimtuma wakapige chicha?...Alishadhamiria bana..........hii bishara ya kusingizia sijui pombe siju shetani mi haiingii kichwani kabisa!
 
Mhh nataman hiyo mimba isingetoka, mana ingebid tu umwambie mkeo. Maana hapa naona unajitahid sana kupambana mkeo asijue,. Unavyohangaika kuomba ushaur, ungefanya hiv pia kabla ya kumcheat mkeo.

Na huyu dada tu aendelee kukusumbua,maana hii itakukumbusha ulikosa ili usije ukarudia siku nyingine. Angenyamaza nadhan ungekuwa umeshachovya kwa mwingine.

Nimpenda bure yaani utakoma chovya chovya, wengine hawaguswi, ukome.

Na uende ukamwombe msamaha mkeo!!

Ni hayo tu!
 
Kabla hawajaenda kupiga chicha, ni pombe ndo ilimtuma wakapige chicha?...Alishadhamiria bana..........hii bishara ya kusingizia sijui pombe siju shetani mi haiingii kichwani kabisa!

Mwenyewe unaelewa ukipiga chicha unakuwa mtu si wa kawaida tena

Chicha linafanya umuone Eliza kama Malikia na hapo hapo unaanza mahesabu ya haraka haraka.

Mpwa chicha limenifanya leo niamka Mlandizi bila kujijua
 
Fikiria mmeo anakuja kukwambia alikuwa anamega mdada flani na amepiga mimba kabisa utapokeaje ujumbe huu?

Hapo mzazi kufa na tai shingoni
 
Fikiria mmeo anakuja kukwambia alikuwa anamega mdada flani na amepiga mimba kabisa utapokeaje ujumbe huu?Hapo mzazi kufa na tai shingoni
Kumega ni kumega tuMimba hata dkk haichukui bwana,kwani mpka umege sana?Ili asamehewe lazma akamuombe msamaha aliyemkosea
 
Dada Lizzy, naona umetutoa kwenye thread, yaani wewe kwa kusoma tu hiyo stori ya ndugu yetu huyo unakuwa mkali kama wewe ndo umeumizwa?, Nadhani msamehe mshauri nini afanye kuepukana na dhahama iliyomkuta, na achukue hatua gani ili asirudie!
Asante ndugu yangu Edo kwa kunielewa.
Unajua maisha ni mzunguko, tatizo la mmoja ni kicheko cha mwingine
 
asee pole mkuu...hata mm hii kitu iliwahi kunitokea.....kata kabisa mawasiliano ikibidi hama kabisa maeneo aliyokua anafikia...then badilisha namba ya simu manake inavyoonekana amekupenda kweli mkuu ana ana kama ukichaa hv

Thank you ndugu, unajua tatizo hili laweza kumtokea hata mtu mjanja kabisa ilimradi kuna dada amekupania.
Omba lisikupate na ukakutana na kichaa kama huyu.
Katika hii stori wengine wanaona ni hadithi zisizo na ukweli, lakini limenitokea na kwa bahati au bahati mbaya nina kauwezo.
Kirahisi, najua huyu bibie anatafuta maisha na kwa umri wake si rahisi kupata mtu wa kumuoa.Hivyo anataka kulaizimisha unyumba-ndogo.
Hili lipo sana mijini.
Nitazingatia ushauri wako.
 
Fikiria mmeo anakuja kukwambia alikuwa anamega mdada flani na amepiga mimba kabisa utapokeaje ujumbe huu?

Hapo mzazi kufa na tai shingoni
He he he
Asante sana Fidel kwa ushauri wako.
Kwa kifupi nikifikiria tu mke wangu akipata hizi habari , magoti yanagongana.
Lakini wambea wengi, naomba humu JF kama kun mtu anayemfahamu mtu kama huyu asimwambie mke wangu.
 
I wish ungekuwa na mke kama mimi. Mimi mume wangu akiniomba msamaha kwanza hapatakalika kwa muda. Ila waklahi tungeshirikiana kumwadabisha huyo mshenzi. Jamani nyie wadada wenzangu temeeni mate chini huko mitaani wadada wenzetu ni balaa yani wako kimawindo zaidi.

Mimi nimekuelewa kaka kwani nina uzoefu na haya mambo and will always be on my husband's side kwani najua mna majaribu mengi sana toka kwetu kaka zetu.

Nina similar experience sitaki kusimulia hapa na nimejifunza kuwa kusamehe ni kitu muhimu sana kwenye ndoa. Kama mkeo ni muelewa (kama mimi) mkalishe chini umwambie kwani nakuhakikishia kaka huyo kicheche lazima atajamtafuta mkeo na kumwambia yote na uongo juu ili akuharibie maana umesema mwenyewe ni kichaa. Tell your wife the truth; then muanze rasmi kumshughulikia huyo mshenzi.

Mume wangu kuna kicheche mmoja alitaka kublackmail kama huyo ila uzuri wa mume wangu si msiri so we worked things out together. Ameniuzia kesi kwa hiyo i am now dealing with this stupid lady!
 
Reactions: EMT
pole sana,kuna wanawake ving'ang'anizi! Ila huyo dada shida yake ni pesa. Cha msingi ignore. Hv kuna uwezekano wj kupata statement ya simu kwenye msg ili kuwa ni ushahidi? Na cha muhimu mkwepe na mu-ignore.

Ila ujifunze na ukome kuchovya nje. Wanaume mridhike na wake zenu! Wanawake wa nje wako kimaslah tu!
 
Labda ni mtu mmoja kapika story zote mbili...

hivi anakaa barabara ya ngapi huyu jamaa?
lakini sishangai, wajasilia mali wanaume wa mlimani(lushoto) wanasifika sana
kwa kuwa na nyumba ndogo. labda hapa anatangaza nafasi nyingine
 
He he he
Asante sana Fidel kwa ushauri wako.
Kwa kifupi nikifikiria tu mke wangu akipata hizi habari , magoti yanagongana.
Lakini wambea wengi, naomba humu JF kama kun mtu anayemfahamu mtu kama huyu asimwambie mke wangu.

Sasa kamanda Majoja unajuaje huo ujauzito ni wako?

Usije ukawa unahudumia mimba ya The Boss ukajua wewe ndo umepanda mbegu.

Tafadhari wife wako hakikisha hajui hii kitu akijua tu mdudu anaingia kuvuruga ndoa yenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…