Nimeiona hii thread nikaurukia haraka, maana mimi huwa sipendi kuanzisha thread but sikiliza hii; mwezi wa tatu mwaka huu 2011 nilipata kazi mahali fulani, nikaenda kuripoti mwezi wa nne tarehe fulani hivi, nikapewa mikataba na yote yanayohusika ila salary wao wanapitishia NMB account yangu ni NBC so ikabidi nianze kufuatilia NMB, nikaenda kwa Mjumbe akala buku mbili kwajili ya barua, mtendaji akala buku tatu jumla tano, kufika NMB Mlimani City wakasema hawataki zile barua wanataka barua ya mwajiri....nikarudi kwa mwajiri akaandika barua ya utambulisho, nikaenda tena wiki iliyofuata kufika palepale wakasema wanataka kitambulisho changu cha kazi/kadi ya mpiga kura au pasport, kwakuwa ndio nimeanza kazi sikua na kitambulisho nikabeba pasport kufika wakakuta jina moja ni tofauti (other given names) ambalo liko kwenye pasport wakagoma, nikaenda nikarekebisha, nikarudi tena, wakasema wanataka barua ya kunitambulisha toka kwa mwajiri na barua ya mwajiri hapa ikabidi niulize hio barua ya mwajiri aandikaje? mmmh nilivyojibiwa nadhani yule binti alikuwa na ..... haya nikaondoka. Nikaenda nikaja kurudi tena, kufika wala hawakushughulika hata kukagua fomu zangu wakasema hakuna mtandao/mtindio, nikanuna tu kimoyomoyo nikaondoka.
Nikahama tawi so ikabidi nikaanze process upya, kufika kule nako wakagomea ila barua ya mwajiri na barua ya kitambulisho cha muda wakati kitambulisho changu kinafanyiwa kazi wakasema wanataka vitambulisho tu vya kazi tu. mmh nikachoka, nikamia tawi la Magomeni sasa wiki tatu zilizopita (August mwanzoni) nikajiandaa vizuri sana this time nikaenda jumamosi bhana si unajua katikati ya wiki lazima uwepo kazini, kufka nikakutana na dada mmoja kavuta mdomo usiambiwe, akanijibu kwa kifupi sana, leo jumamosi hatufungui account asipojua kuwa yale matawi mengine yote nilikokwenda nilienda jumamosi, haya nikarudi nikaisubiri jumatatu (yaani jana) ikabidi nichelewe kazini nipitie magomeni tena kufika akanijibu simple tu, "leo hatufungui account hadi baada ya sikukuuu..." shenzi, nikataka nimtukane ila nikawa mpole tu, nikamkumbusha kuwa jumamosi alisema jumatatu, akawa ameshasahau kuwa alisema hawafungui account jumamosi yeye akasema eti alinijibu vile kwakuwa kulikuwa na matatizo ya network.....sasa nasubiri Idd iishe ijumaa niende sijui wataniambiaje huko. Yaani sikushauri hata uende huko, uende ukiwa umelazimika kwenda kama mimi, hebu imagine kuanzia April hadi september sijafungua account.