It is appalling kuona anaeyongoza TAKURURU ni Dk lakini anachemka hakuna mfano. anaongea kama mwanasiasa mwerevu! Mambo ya Rushwa iliyokithiri amaayo huwezi kuitenganisha na UFISADI Uliozagaa Tanzania still anasema kesi 10 ZITATAJWA MWAKA HUU!! He makes me feel sick.
hebu soma hii hapa chini. Sioni mantiki Mpaka apikiwe na apewe allowance ya seminar ndiyo ayaseme haya hapa chini.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuizua Rushwa Nchini, (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, amesema uchunguzi wa kesi kubwa 10 za rushwa utatangazwa mwaka huu.
Alisema kuwa kati ya kesi tano matokeo yake yanatarajiwa kutangazwa baada ya mwaka wa fedha wa serikali ambao unamalizika Juni 30, na zingine ifikapo Desemba, mwaka huu.
Hayo alisema jana wakati akifunga semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la African International Group of Political Risk Analysis (PORIS) kuhusu maboresho ya Utawala Bora dhidi ya kupambana na rushwa iliyofanyika, Bagamoyo mkoani Pwani.
Dk. Hosea alisema uchunguzi wa kesi zimefikia katika hatua nzuri ya kukamilika na matokeo ya kwanza yanatarajia kutangazwa mwishoni mwa mwaka wa fedha.
Alisema PCCB itachunguza kesi zote ambazo zinawakabili baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu serikalini ambao wanahusika na kuingia mikataba mibovu ya serikali ambayo inadaiwa rushwa ilitumika katika kupitisha mikataba hiyo.
Dk. Hosea alisema taasisi hiyo haijalala usingizi kuhusiana na tuhuma za rushwa ambazo zinawakabili viongozi ambazo zingine zimeibuliwa na wabunge.
Aidha alisema kuwa, wananchi wasifikiri hawafanyi lolote dhidi ya tuhuma za rushwa na kuongeza kwamba jamii inatakiwa kushirikiana na chombo hicho ili kuweza kutoa taarifa za rushwa.
Dk. Hosea alisema kuwa baada ya uchunguzi wao watapeleka uchunguzi wao mbele ya vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
Hata hivyo, aliushukuru Ubalozi wa Ubelgiji kwa ufadhili wa fedha kutoka PORIS katika kuenzi utawala bora nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa PORIS, Bw. Prince Bagenda, alisema kuwa semina hiyo inafuatia matokeo ya Brussels yaliyofanyika Machi 14-15 mwaka jana nchini Ubelgiji kuhusiana na maboresho ya Utawala bora na jinsi ya kupiga vita rushwa.