Infact Ufisadi haupo tu katika Ngorongoro hata katika shirika la hifadhi a Taifa, TANAPA. Na huu umekuwepo muda mrefu sana. Kwanza kulikuwa hakuna sababu ya msingi ya kuitenga Ngorongoro kutoka TANAPA na kutengeneza shirika lingine. Hapo awali ngorongoro ilikuwa inahifadhiwa na TANAPA na ilikuwa sehemu ya mbuga ya Serengeti.
Watanzania kila siku wanajivunia kuwa tuna maliasili za wanyamapori, ohh utalii lakini kimsingi hizi zinawanufaisha watu wachache sana. Mashirika yote haya mawili hayachangii chochote katika hazina ya Taifa zaidi ya kodi. Hata hivyo kuna mikakati inafanywa ili wasilipe kodi, eti kwa sababu wanamajukumu mazito.
Wakati idadi ya wanyam inaendelea kupungua siku hadi siku, mwaka jana members wa board ya TANAPA waligawana kifuta jasho cha shilingi Million 20 kila mmoja eti kwa sababu wamevuka lengo. Imagine ma-rangers ambao ndo wanakaa kila siku huko porini na kulinda wanyama, hawakuambulia bonus yoyote. Hizi tasisi mbili pamoja na board zake ni hatari sanaaaaaa.