Tunatakiwa kuwa wajanja, tuunganishe uchumi wetu kwa uchumi wa makampuni ya madini, mfano tujipange kwa makusudi kuhakikisha tunaanza kutoa huduma (zile tunazoweza, kama vyakula, supplies of local produce n.k.) ili tuweze kulazimisha kiasi fulani cha pesa kibaki Africa - Tanzania kwa njia ya biashara na utoaji huduma. Inasikitisha kuona bidhaa kama maziwa yanaagizwa nje ili yatumike migodini wakati migodi yote iko kanda ya Ziwa - eneo linaloongoza kwa wingi wa Ngo'mbe!