Jamani Serikali, huku sio kuwaibia watanzania?

Ufunguo

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2012
Posts
330
Reaction score
231
Kama utakumbuka vizuri katika kikao kilichopita cha bajeti ya serikali bungeni Dodoma, wizara ya fedha ilipeleka mswada bungeni wa kurekebisha viwango mbalimbali vya ushuru ikiwemo ule wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi hususani magari. Kutokana na mapendekezo hayo, gari yenye umri zaidi ya miaka 8 tangu kutengenezwa ilitakiwa kulipiwa ushuru wa uchakavu ambao ni 20% ya CIF. Sasa kabla ya mapendekezo hayo hayajaridhiwa na bunge, tayari mamlaka ya mapato TRA wakaanza kukusanya ushuru kwa viwango vipya vilivyokuwa vimependekezwa. Bunge halikukubaliana na maendekezo hayo na kuamuru ushuru kwa magari uendelee kutozwa kama ilivyokuwa hapo awali , yaani utozwe kwa magari yaliyokuwa yana umri wa miaka zaidi ya 10 tangu kutengenezwa.
Mimi niliingiza gari katika kipindi hiki cha mpito (mwanzoni mwezi 8 mwaka huu) na gari yangu ilikuwa ya mwaka 2003. TRA wakanitaka nilipie pamoja na ushuru mwingine, ushuru wa uchakavu kulingana na mapendekezo ya mabadiliko ya ushuru yaliyokuwa hayajapitishwa na bunge.
Sasa baada ya serikali (bunge) kukataa hayo mapendekezo ya Wizara ya fedha kuhusu kutoza ushuru wa uchakavu kwa magari hayo, je ushuru wa uchakavu ambao nililipa naweza kurudishiwa?. Kama siwezi kurudishiwa, serikali haioni kama imewaibia wananchi fedha zao?. Na je kwanini TRA wanaanza kukusanya ushuru wakati bunge halijaridhia mapendekezo hayo?, ni sheria gani inayowaruhusu TRA kuanza kusanya kodi wakati hata bunge halijaridhia mapendekezo ya mabadiliko ya viwango vipya vya ushuru?. Je naweza kuiburuza serikali mahakamani kwa kosa kama hili?, nasema hivyo kwa kuwa ni watanzania wengi walioathirika na ushuru huu.
Naomba ushauri wa kisheria na ki-taratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…