watanzania sasa wameamka kutoka usingizini kuidai katiba mpya inayoendana na hali halisi ya wakati uliopo lakini ni suala la kusikitisha kuwa watanzania walio wengi hata rangi ya katiba wanayoipiga vita kuwa imepitwa na wakati hawaijui je, hata kama wakibadilishiwa katiba hiyo kuna uhakika gani kuwa mambo hayatabaki kuwa yaleyale wanayoyakataa sasa hivyi? Hapa suala ka msingi ni kudai katiba hii iliyopo itafasiriwe kisha wagundue makosa yaliyopo katika katiba hii na sio kupiga kelele kwa kuwasikiriza wana siasa bila kupima uzito wa jambo ndio wasimame kwa miguu yao wakiwa wanajua wanachokidai kiko je, na wanacho kikataa kiko je.