Tetesi: Jamani Tuache Uanaharakati kwenye masuala ya Kitaalam..

Tetesi: Jamani Tuache Uanaharakati kwenye masuala ya Kitaalam..

blix22

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
213
Reaction score
645
Jamani nawasihi tuache uanaharakati kwenye mambo ya kitaalam hasa pale tunapokuwa hatuna ufahamu wakutosha kwenye jambo husika. Lakini pia kwenye jambo lenye maslahi mapana ya jamii kama mfumo wa pensheni siku zote tujifunze kulijadili kwa kuzingatia mapana yake, tusiwe wabinafsi. Kabla ya kubeza mabadiliko yaliyofanyika kupitia Sheria Na. 2 ya mwaka 2018 tunapaswa kuelewa mambo yafuatayo:
1. Mfuko wa Pensheni siyo benki ni mfuko kwa ajili ya mafao ya uzeeni. Mafao yake yamekusudiwa kumsaidia mwanachama pale anapopoteza uwezo wa kujipatia kipato kwa sababu ya uzee, kupata maradhi au ulemavu utakaopelekea kupoteza uwezo wa kufanya kazi. Mafao haya pia yanakusudia kuwasaidi warithi/wategemezi wa mwanachama au mstaafu pale anapofariki.

2. Mfuko wa pensheni ni wa wanachama wenyewe . Hivyo, uhai na uendelevu wa mfuko unategemea uchangiaji wa wanachama na mfumo wa ukokotoaji na ulipaji wa mafao. Ni lazima kuwe na uwiani halisi baina ya kiwango cha uchangiaji na kiwango cha mafao yanayolipwa. Tofauti na hapo utakuwa na mfuko wenye sura ya "Desi/Upatu" ambapo mfuko utaishia kulipa wanachama wachache na waliowengi watakosa mafao:

3. Mafao ya pensheni yanakusudiwa kuwa mbadala wa kipato/mshahara ambao mwanachama alikuwa akipata kabla ya kustaafu. Ndiyo maana sehemu nyingine duniani hakuna utaratibu wa kulipwa kwa mkupuo, badala yake pensheni yote (full pensheni) hugawanywa na kulipwa kwa kila mwezi (monthly pensheni). Lengo ni kuhakikisha kwamba kiasi cha pensheni ambacho
mwanachama anakipata kinamwezesha kuishi maisha yanayofanana na maisha aliyokuwa akiishi akiwa kazini. Hii ndiyo sababu ya Kanuni za 2014 na 2018 kuweka mgawanyo wa pensheni wa asilimia 25% (mkupuo) na 75% (pensheni ya kila mwezi). Kwa utaratibu huu malipo ya pensheni ya kila mwezi yataongezeka.

4. Ni muhimu pia kutambua kwamba Kanuni za Mafao za mwaka 2018 ni mwendelezo wa Kanuni za Mafao za Mwaka 2014 ambazo zimekuwa zikitumika kwa wanachama wa Mifuko ya PPF na NSSF na pia kwa Wanachama wa Mifuko ya PSPF, LAPF na GEPF walioajiriwa kuanzia Julai, 2014. Hivyo, siyo Kanuni mpya kama ambavyo baadhi ya watu wanajaribu kupotosha.

5. Kuhusu ukomo wa mafao ya mstaafu. Mstaafu atapokea mafao yake mpaka mwisho wa uhai wake. Hata baada ya mstaafu kufariki, warithi/wategemezi wake wataendelea kupokea mafao kwa kipindi cha miaka mitatu bila kujali mstaafu huyo amepokea pensheni kwa miaka mingapi. Hii ni tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya mabadiliko ambapo mafao ya mstaafu yalikuwa yanakoma siku mstaafu anapofariki.
Hivyo, taafsiri kwamba mstaafu atapokea pensheni kwa miaka 12.5/15.5 tu siyo sahihi hata kidogo na ni upotoshaji wa makusudi. Kipindi hicho kimewekwa kwa madhumuni ya ukokotoaji wa mafao tu. Ni muhimu pia kufahamu kuwa vipindi hivyo pia vilikuwepo kwenye kanuni zilizopita lakini wastaafu wameendelea kupokea pensheni zao hata baada ya kumalizika kwa vipindi hivyo.

TUSIWE WABINAFSI, MIFUKO NI YETU SOTE NA INAPASWA KUENDELEA KUWEPO KWA MASLHAHI YA WANACHAMA WOTE
 
"... mfuko wa mafao sio Benki.... '' hii elimu wape wanaokopa kujenda Kigamboni Bridge, Udom na miradi mingine kabla ya kuwaambia hivyo pensioners
 
Back
Top Bottom