Jamani tujaribu kuwa wawazi katka mahusiano!

Mapenzi ya dhati yalikuwapo zamani kwa sasa tunaongopeana tu!
Hio ni kweli me nimewahi kukutwa na hili nilikuja kustuliwa ijumaa kwamba jmos jamaa anaoa na alhamis alienda kwenye send off na siku hyo tulikuwa pamoja akaniambia kuna harusi ya mfanyakazi mwenzao anaenda eti hajapewa kadi anaenda kama mwanakamati hawezi kwenda na mimi kumbe ndo alikuwa anenda kwenye sendoff yake duh! me sina hili wala lile. wanaume Pu!
 
Mhh!!! yani wewe, yani mpaka jamaa anaoa wewe hujui?
Labda kama mlikuwa mnakutana kungonoka tu! na mliuwa hamna time pamoja!
 
Pole sana ndugu yangu. Ni mambo mazito sana na wengi wetu hatuwezi kuyaelewa kwa uzito ule kwa kuwa kwetu tulio wengi tunaishia kusimuliwa. Kwa ufupi ni unyama na uuaji kwani kama mtu aliyepatwa na hilo tatizo hatakuwa strong kukabiliana nalo anaweza kuwa kichaa na maisha yake yakaishia hapo. Nakupongeza kwa kuyahimili na kusonga mbele.

Mhh!!! yani wewe, yani mpaka jamaa anaoa wewe hujui?
Labda kama mlikuwa mnakutana kungonoka tu! na mliuwa hamna time pamoja!
Kumbe hata wewe umeona. Hapa kulikuwa na tatizo. Mawasiliano kuhusu matarajio na lengo la kuwa kwenye mahusiano yalikuwa ICU! Ni muhimu watu wakawa wanaongea kwa nini wako pamoja na watakuwa hivyo hadi lini! Ila mara nyingi naona kama dada zetu wanategemea hisani ya akina kaka ili watangaze nia. Hata hivyo inabidi kukumbuka kuwa wanaume wengi wanaingia kwenye mahusiano kumaliza kiu ya ngono tu, na mengine ni matokea.
 
Mhh!!! yani wewe, yani mpaka jamaa anaoa wewe hujui?
Labda kama mlikuwa mnakutana kungonoka tu! na mliuwa hamna time pamoja!
Tulikuwa tunakutana kila mahari ila alienda kuoa nje ya mkoa me ninge juajae na kila nilipo muihitaji alikuwepo na mipango ya baadae ilikuwepo anyway woote mnao tetea ni wanaume ngoja niachane na nyie wanaume Pu!
 
Pole salha, umenikumbusha shost yangu mmoja nilipokuwa chuo alikumbwa na mkasa kama wako aliponea chupu chupu kudisco
wanaume acha bwana
 
Labda tokea mwanzo hamkupeana definition ya wazi ya uhusiano wenu..... Mwenzio anajua ni friends with benefits wewe wajua ndo wa maisha
 
...LOL! kuna watu wamedata haki ya mungu, ha ha ha haa....No comment hapa acha nicheke tu.
 
Nampa pole huyo dada. Lkn wanaume achana nao kabisa...they can mess up ur life if u let them. Advise, have courage and willpower to continue maana its not the end of the world. Been in that same boat but the difference is I came out stronger...and since then my focus is about myself and no complications.
 
Ni ukatili. Hakuna jingine. Ukiona kuwa uliye nae itafika siku utammwaga, bora ufanye hivyo kungali alfajiri. Usiruhusu mapenzi (ambayo ni ya upande mmoja) kumea. Kama una hofu ya mapoozeo nenda kanunue au ujichue kuliko kumtesa mwenza. Tatizo ninaloliona kwa wengi hata kufikia mifarakano ya kutisha ni kutopangilia mapenzi na kujua kuwa nimpende nani na kwa nini. Wanaachia hisia zinawatawala. Siku hisia zinafeli breki inakuwa ni kuangamia tu
 
Labda tokea mwanzo hamkupeana definition ya wazi ya uhusiano wenu..... Mwenzio anajua ni friends with benefits wewe wajua ndo wa maisha

Bora basi uhalisia wa mambo ungekuwa japo karibu na hapo. Naambiwa ukiweka hilo wazi mapema,chances are 'hakuna kitakachoendelea hapo'...lol

Binafsi naona tatizo ni unafiki katika mahusiano hususan ya kimapenzi. Kwanini tunashindwa(wanaume na wanawake) kuwa wakweli,kuhusu nia na malengo yetu, kwa nafsi zetu na wenzetu(this goes with living with whatever the consequences thereof)?Labda tuanzie hapo......
 
Hairuhusiwi kusimama wala kufanya biashara yoyote hapa. Ni Amri by Utawala

Stukeni wanawake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…