Jamani ukipenda Ua basi penda na boga lake

bacha

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2010
Posts
4,282
Reaction score
797
or the vice versa is true!!!!!!

Kuna jamaa mmoja alisikika akilalamika mbele ya wenzake;

Nanukuu,

''Mke wangu toka tumefunga ndoa amebadilika na kuwa mtu wa kununa na kujifungia ndani kila wakati hasa pale ndugu zangu wanapokuja kunisalimia kwangu. Ukizingatia kuwa mimi ndo kaka mkubwa katika familia yetu na wazazi wetu wote (Baba na Mama) wameshafariki, kwahiyo nimebaki kuwa msaada mkubwa kwao."

Mwisho wa kunukuu.

SWALI: Hivi ni kwa nini kwenye ndoa nyingi akina mama huwa wanagombana au kushindwa kukubaliana na uwepo wa ndugu wa mume nyumbani tofauti na akina baba? Ikitokea tu ndugu wa mume wamekuja nyumbani, basi mama hubadilika tabia, yaani ule uwajibikaji wa kila siku unapotea ghafla na kutwa nzima ananuna nuna tu!tafadhali naomba nisisitize, sio akina mama wote
(nimesema kesi nyingi hapa utakuta ni akina Mama Vs ndugu wa mume na sio Baba Vs ndugu wa mke!!!!)!!!!!!!!!!!!!


Samahani dada zangu, siwapondi ila naelezea hisia zangu!!!!!
 
kweli hii tabia ni common sana kwa akina mama.
Nashindwa kutoa jibu la moja kwa moja ina nahisi wasichana kama tuna wivu/tunabold vitu vidogo vidogo kuliko MEN

Tena bora wawe ndugu wa kiume lakini mama mkwe/mawifi huwa panachimbika.
Kuna mdada flani hajaolewa ila ameshamwonya mchumba wake kuhusiana na dada zake wakati hao dada wanaishi mji tofauti na wanajitegemea
 
ukiingia kwenye familia ya watu unakuwa na kazi ya ziada kutoleta feelings tofauti. inawezekana mke anajiskia tu kupumzika ama kufanya shughuli za chumbani kwake,ila kwa vile ndugu wana wasiwasi wanahitimisha kuwa wanakimbiwa.mume ka upendo anaweza kumuelimisha mkewe kuwa kukiwa na ageni jitahidi ku-hang around ili isilete mtazamo hasi.mm mama mkwe ndo alinifundisha hii 'asiyekua na time na ww na ww mpetezee.anayekuonesha upendo na w muoneshe'. so kama ndugu wa mume ananipotezea,mi na-chill tu,hatushushani sukari.
 
this is how it start dear
next time unawakuta sebuleni na kaka yao unawasalim wanajifanya wako bize kwenye mazungumzo
 
mpendwa, yaani nitawasalimia na kufanya yanayonihusu manake salamu haiuzwi! tena na kumuambia dada menu na abadilishe bedsheets kwa ajili ya wageni! watazunguuka huko misho wa siku anagundua mbona kwa wifi ndo pa kuponea?na akija mtu kwangu wala simuulizi y alikuwa anani_ignore!life is how u make it. unajua hata ww una ndugu zako enye moods,dawa yao unawaacha they come around at some point! as long as no physical attack, na hajaongea neno baya mbele yangu, watapata smile na pengine i ont dig out my pocket for someone ignoring me!ila hata anisemee hukooo,siulizi atashangaa menyewe huyu dada vp? kesi ndo zinaleta mgongano!very simple trick,makes the world a better place my dear!
this is how it start dear</p>
<p>next time unawakuta sebuleni na kaka yao unawasalim wanajifanya wako bize kwenye mazungumzo
 
 
Shemeji yangu hana matatizo sasa sijui kwasababu kwenye familia yetu wote wanaume msichana mmoja tu
 
Ni kweli mara nyingi akina mama tunakuwa na tabia hii, nami kama mdau aliyetangulia, nashindwa kutoa jibu la moja kwa moja juu ya nini kisababishacho hali hii. Labda mke anakuwa na matarajio kuwa sasa ameolewa atakuwa na nyumba yake akiwa na privacy na hasa kuamua mambo yahusuyo nyumba yake. Sasa anajikuta hata pa kupita tena hamna, akigeuka huku mama mkwe, kule wifi, pembeni shemeji basi mtafaruku tu. Hata kukatiza na kanga tu haiwezekani tena (haa haa...).

Mara nyingine akina baba wanajisahau kuwa sasa ameoa na ama majukumu pia ya familia yake mpya, kwa hiyo ku-balance anashindwa. Matokeo yake anafanya vitu na maamuzi kama vile alipokuwa nyumbani kwa wazazi wake, na hajaoa. Nimewahi kushuhudia fedha ya matumizi ya ndani anaachiwa mama mkwe badala ya mama. Sasa hii hupelekea kitu kama ushindani kati ya mama mkwe na mke, utafikiri wote wanagombea mume, kumbe kwa mmoja wao ni mtoto wa kuzaa. Na mara nyingine mama mkwe ni kama anakuwa hajakubali or rather 'anagoma' kumuachia mwanae kuwa sasa naye amekuwa mtu wa majukumu mapya. Bado anamuona kama 'my sweet little boy'.

Kama kuna uwezekano, basi mume aache familia yake (ya kuzaliwa nayo) iliko, yani asihamishie familia yake yote kwake. Kama yeye mke na mume tu wana uwezo wa kupishana na kukwaruzana, sembuse hao ndugu wengine? Hii nayo itaepusha vijembe na masimango yasio na lazima kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Na labda niulize swali, kabla hamjaoana, hiyo familia ilikuwa inaishi wapi mpaka ihamie kwako ukioa? Kama ni wa kuja na kusalimia, hiyo sioni kama ina shida, labda tu huyo mke awe ana hulka yake tu ya kununia watu. Ila nako kusalimia sio tena kama kuhamia, watu mwezi wanasalimia tu jamani?

Kumbukumbu yangu wakati tuko wadogo, baba yetu alikuwa hakubali kabisa twende kwa dada yetu, ambaye alikuwa ameolewa. Swali lake kubwa, wamekuita uende? Kwa hiyo tukajikuta hatuna utaratibu wa kufunga tu mizigo kwamba unaenda sijui kumsalimia mjomba sijui shangazi. Mpaka tuende, basi zimeshapita protokali utafikiri tunaenda ikulu.
 
Reactions: SMU
Hao ndugu wanatafuta nini kwa kaka yao hawajaolewa hao wakaishi na waume zao nazungumzia mawifi

Nitarudi ngoja kwanza nikumbuke mawifi zangu na mashemeji.

Ha ha ha ha Bacha bana leo yamekukuta yapi tena mkeo kanunia Dada zako (Joke)
 
tunashukuru kwa maoni yenu hapa mmetupa picha hata sisi ambao bado hatujaoa.........
 

Nalisubiri hilo jibu hapo juu,
kwani ndilo haswa litatufunua hapa!!!!!
 
Hao ndugu wanatafuta nini kwa kaka yao hawajaolewa hao wakaishi na waume zao nazungumzia mawifi

Nitarudi ngoja kwanza nikumbuke mawifi zangu na mashemeji.

Ha ha ha ha Bacha bana leo yamekukuta yapi tena mkeo kanunia Dada zako (Joke)

jamani haondugu ndo wanamtegemea huyo mkaka,
na bahati mbaya wazazi wao wote wameshafariki!!!!
unasemaje hapo?
 

Huwa inakuwa mbaya zaidi kama anayekuja kutembelewa hali yake kiuchumi ni bora (au inaonekana bora) zaidi kuliko hao wageni! So sababu mojawapo ni ya kiuchumi zaidi.

Nyingine ni tabia za hao ndugu wanaokuja kutembea....kama ni watu wenye 'mdomo' mara nyingi wakija mama mwenye nyumba anajua wamekuja kutafuta cha kusema!
 
Shemeji yangu hana matatizo sasa sijui kwasababu kwenye familia yetu wote wanaume msichana mmoja tu

Ok, kwani ulishawahi kukaa kwa muda kidogo hapo kwa brother?
 


ohooo......... kumbe eeeee...........................
 
this is how it start dear
next time unawakuta sebuleni na kaka yao unawasalim wanajifanya wako bize kwenye mazungumzo

Labda wakati mwingine inategemea na hiyo salamu uliitoaje.......
labda kama uliitoa huku sura na shingo vyote vinaangalia magharibi,
na wao wako mashariki, kweli kuna salaam hapo?
 
 

Asante kwa angalizo na ushauri Dina!!!!!!
lakini bado unaamini kuwa ukipenda ua basi ni vema,
upende na boga lake?
 


Kwahiyo SMU,
unataka kuniambia hizi sababu zinaweza kumfanya mama,
ajifungie chumbani na kuzanza kununa nuna eeee?
 
jamani haondugu ndo wanamtegemea huyo mkaka,
na bahati mbaya wazazi wao wote wameshafariki!!!!
unasemaje hapo?

Yaani ukoo mzima uhamie kwangu hiyo hapana awasaidie wakiwa huko huko kwao sio kuja kujazana nyumbani kwangu ukoo wote nitawanunia kwa sana tu (joke) bana ha ha haha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…