Kwani hawa vijana ulikuwa unaishi nao kabla ya wazee kutangulia mbele za haki? Nafikiri na wewe kaka yao uwe na malengo nao, coz kama asubuhi mpaka jioni wametega miguu juu ya coffee table wanabadilisha channel za TV tu, itakuwa shida mbele ya safari. Si ajabu mmegawana majukumu kwamba wewe baba hela yako utakuwa unashughulikia project kubwa kubwa (mkwara wenu huu) na mama yeye alishe nyumba. Mama naye kuhakikisha familia inakuwa komfotable anakazana kubadilisha mboga huku hata yeye hao wadogo wa kuja kuwaweka hapo na yeye anao na hamna yeyote anayemsaidia kuwalea, ukiwemo wewe mume wake! Sasa fair play hapo iko wapi?
Umenikumbusha shoga yetu mmoja aliyeambiwa na mumewe aache kazi ili amhudumie mama yake mzazi aliyekuwa amekuja kwa ajili ya shida ya hospitali. Mume wala hajataka kufikiria kuwa, mkewe naye ana mama ambaye anamtegemea, hiyo kazi akiacha itakuwaje?
Kwa hisia hii yamekukuta pole. Ila haya maneno yamuingie Bacha na ubishi wake
oraiti Dina,sasa unamwambiaje huyo bwana
awafukuze hao ndugu au,
kwani yawezekana wapo pale kwa mahitaji mbalimbali,
shule, ugonjwa n.k.
sasa jamani ndugu wasiongee kabila lao,
eti kwakuwa shemeji yao haelewi hicho kiluga?
huyo mwanamke si aliolewa akijua kabisa ameolewa kwenye kabila gani,
sasa leo hao shemeji zake kuongea kiluga inamkwaza vipi?
Niseme wafukuzwe ili wote wanitenge na kutaka kuniua? Kama alivyosema mdau mmoja, wape nyavu za kuvulia kaka sio samaki ambaye ushamuunga na viungo vyote! Mimi ninachojiuliza hao vijana ulikuwa nao siku zote au wanahamia na nguo moja moja kwenye mfuko mpaka makabati yanajaa? Bacha usije ukafikiri mie 'mpalestina' sana when it comes to ndugu wa mume, hapana, bali sipendi watu wafanye nyumbani kwangu ghetto! Na hii ina-apply kote, hata kwa ndugu zangu mwenyewe, tena hao ndio sitaki lawama kabisa. Ninao wadogo wanne ambao wote nimehangaika nao mwenyewe, lakini wakiwa kwa mzazi wao (mama, ambaye nashukuru mungu kwa uwepo wake). Na sijawahi kuongezewa ada hata punje na baba mwenye nyumba, lakini kuweka kambi kwangu hapana, unless kuna shida maalum, coz sitaki pia kumkwaza mwenzangu.
sasa jamani ndugu wasiongee kabila lao,
eti kwakuwa shemeji yao haelewi hicho kiluga?
huyo mwanamke si aliolewa akijua kabisa ameolewa kwenye kabila gani,
sasa leo hao shemeji zake kuongea kiluga inamkwaza vipi?
Labda Bacha ataelewa sasa maana mbishi kama nini
Unajua Dina sio kwamba naweza kukuona wewe ni mpalestina,
hapana , hata kidogo!tunajaribu kushea aideas hapa ili tuone maisha kwa ujumla tunayafanya yawe ya furaha kwa kiasi gani,
Naelewa kabisa kuwa maisha yetu ya kitanzania yanafanana sana, extended families!
yawezekana kwako ikawa ngumu sana kuihi na ndugu lakini kwa mwingine kukawa hamna namna ni lazima awe nao!!!!
Hii ni kutokana na mifumo yetu ya kimaisha kwa ujumla!
sasa, hebu angalia hii!wazazi wamefariki,
vijana walikuwa wanasomeshwa na mzee,
wewe kaka mkubwa angalau unakipato fulani, na automatically utayabeba hayo majukumu!
unaonaje basi hao ngugu 2, au 3 wakija kwako waendelee na shule na wengine ,
kuwatengenezea misingi ya maisha yao?
ukizingatia kimbilio la mwisho ni kwako!!!
sasa jamani ndugu wasiongee kabila lao,
eti kwakuwa shemeji yao haelewi hicho kiluga?
huyo mwanamke si aliolewa akijua kabisa ameolewa kwenye kabila gani,
sasa leo hao shemeji zake kuongea kiluga inamkwaza vipi?
Bacha wewe lazima utakuwa kabila fulani hivi sitaki kulitaja
Maana unatetea uongee kilugha wewe na wadogo zako mkeo hasikii hivi utajisikiaje kweli
Mimi nampenda mke wangu siwezi kumtenda haya kamwe
hapana mkubwa,
sio kwamba mimi ni mbishi kwenye hili,
naelewa kabisa udhia uliopo kwa kuishi na ndugu kwangu,
lakini kaka kuna majukumu mengine ni mazito na hayakwepeki!labda uamue kuwa kauzu tu!!!!!!!
kwani MLIMAZUNZU nani alikwambia kuwa,
ukiongea kiluga ndo utakuwa humpendi mkeo,
jamani hiyo si ni luga tu ya mawasiliano,
na hasa pale maongezi yanapowahusu hao watumiaji wa hiyo lugha!
Kwa hisia hii yamekukuta pole. Ila haya maneno yamuingie Bacha na ubishi wake
or the vice versa is true!!!!!!
Kuna jamaa mmoja alisikika akilalamika mbele ya wenzake;
Nanukuu,
''Mke wangu toka tumefunga ndoa amebadilika na kuwa mtu wa kununa na kujifungia ndani kila wakati hasa pale ndugu zangu wanapokuja kunisalimia kwangu. Ukizingatia kuwa mimi ndo kaka mkubwa katika familia yetu na wazazi wetu wote (Baba na Mama) wameshafariki, kwahiyo nimebaki kuwa msaada mkubwa kwao."
Mwisho wa kunukuu.
SWALI: Hivi ni kwa nini kwenye ndoa nyingi akina mama huwa wanagombana au kushindwa kukubaliana na uwepo wa ndugu wa mume nyumbani tofauti na akina baba? Ikitokea tu ndugu wa mume wamekuja nyumbani, basi mama hubadilika tabia, yaani ule uwajibikaji wa kila siku unapotea ghafla na kutwa nzima ananuna nuna tu!tafadhali naomba nisisitize, sio akina mama wote
(nimesema kesi nyingi hapa utakuta ni akina Mama Vs ndugu wa mume na sio Baba Vs ndugu wa mke!!!!)!!!!!!!!!!!!!
Samahani dada zangu, siwapondi ila naelezea hisia zangu!!!!!
Naonaga kwa aunty yangu yani wakija ndugu za mumewe wanalonga kikwao mpaka wanaondoka na mume wake nae anachangia mana anafahamu mkewe si kabila lake ila habadiliki wala kubalisha hao ndugu zake.
Huwa namwonea huruma sana!!..sasa kama huyu akikimbia kujifungia chumbani naona ni bora kuliko kuduwaa na kilugha cha watu.