Chrizant Kibogoyo
Senior Member
- Aug 12, 2016
- 159
- 81
Hii ni rai kwa viongozi wa klabi ya Yanga kuwa tumechoshwa na matusi ya Msemaji wa watani wetu Haji Manara katika mitandao ya kijamii.
Mara kwa mara amekuwa akipost picha za kuwakebehi wachezaji wetu kuwa hawalipwi mishahara, lishe yao ni mbovu n.k.
Niwaombe viongozi wetu wabuni mikakati ya kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu yetu badala ya kutegemea hisani za mtu mmoja mmoja wabuni namna ya kuwashirikisha wanachama na wapenzi wote katika kugharimia uendeshaji wa klabu yetu bila ya kuteteresha misingi ya klabu kuendelea kumilikiwa na wanachama.
Uongozi ubuni mikakati ya kutumia maendeleo ya Tehama kuwashirikisha wanachama na wapenzi wa Yanga katika uendeshaji wa klabu.
Mathalani naamini klabu ya Yanga haiwezi kukosa watanzania milioni 5 kati ya milioni 40 na ushehe walioko tayari kuichangia angalau Shilingi 2,000/= kwa mwaka na kufanya mapato ya Shilingi Bilioni 10 kwa mwaka toka kwa wapenzi wake. Ni muhimu kiwango cha kuchangia kikawa kidogo kati ya Shs 2,000/= hadi 5,000/= ili kuwawezesha wanachamq na wapenzi wa vipato mbalimbali kuchangia. Kikubwa ni uwepo wa mikakati madhubuti ya uhamasishaji.