Jamani wanayanga tumechoshwa na matusi ya Haji Manara

Chrizant Kibogoyo

Senior Member
Joined
Aug 12, 2016
Posts
159
Reaction score
81
Hii ni rai kwa viongozi wa klabi ya Yanga kuwa tumechoshwa na matusi ya Msemaji wa watani wetu Haji Manara katika mitandao ya kijamii.

Mara kwa mara amekuwa akipost picha za kuwakebehi wachezaji wetu kuwa hawalipwi mishahara, lishe yao ni mbovu n.k.

Niwaombe viongozi wetu wabuni mikakati ya kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu yetu badala ya kutegemea hisani za mtu mmoja mmoja wabuni namna ya kuwashirikisha wanachama na wapenzi wote katika kugharimia uendeshaji wa klabu yetu bila ya kuteteresha misingi ya klabu kuendelea kumilikiwa na wanachama.

Uongozi ubuni mikakati ya kutumia maendeleo ya Tehama kuwashirikisha wanachama na wapenzi wa Yanga katika uendeshaji wa klabu.

Mathalani naamini klabu ya Yanga haiwezi kukosa watanzania milioni 5 kati ya milioni 40 na ushehe walioko tayari kuichangia angalau Shilingi 2,000/= kwa mwaka na kufanya mapato ya Shilingi Bilioni 10 kwa mwaka toka kwa wapenzi wake. Ni muhimu kiwango cha kuchangia kikawa kidogo kati ya Shs 2,000/= hadi 5,000/= ili kuwawezesha wanachamq na wapenzi wa vipato mbalimbali kuchangia. Kikubwa ni uwepo wa mikakati madhubuti ya uhamasishaji.
 

Usijidanganye aliyekuwa anaipa Kiburi na Jeuri ya Pesa Yanga SC alikuwa ni Manji peke yake ambaye sasa karibia 75% ya ' income ' yake kutoka katika Vyanzo vyake tegemezi imeshaguswa na kuathirika.

Kosa kubwa walilolifanya wana Yanga SC ni kumuamini 100% Manji na kumyenyekea kwa kila Kitu hivyo nae akawa anawafanya anavyotaka kwani alishawajua kuwa wana Yanga SC wengi ni ' hamnazo ' Kichwani halafu ' choka mbaya ' sana.

Japo mara nyingi mlikuwa mnatucheka wana Simba SC ila mlisahau kwamba uzuri wa Simba SC kwetu huku kuna uhuru wa kutosha kwa Matajiri wengi kuisaidia Timu tofauti na ilivyo Yanga SC na ndiyo maana utaona kwa mfano Simba SC japokuwa Mohammed Dewji ' Mo ' anaisaidia lakini pia wapo Matajiri wengi wanaoisaidia pia mmoja wapo akiwa ni Mzee Bakhressa ambaye ana Timu yake ya Azam lakini ni mwana Simba SC wa kutupwa.

Manji baada ya kujua tu ameshashika akili Yanga SC kupitia wale Wazee akina Akilimali na karibia 99% ya Kamati ya Utendaji ya Yanga SC sasa akawa anafanya atakavyo na ndiyo maana hadi leo hii Yanga SC inavaa nembo ya QUALITY GROUP lakini Timu / Klabu haijalipwa na haijafaidika na lolote kutoka kwa Manji na Viongozi akina Sanga wamekaa kimya kwakuwa tayari na Wao wameshakamatwa ' Kiakili ' huku na Wao pia wakifaidika na ' mtonyo '

Manji ndiyo aliwakosanisha wana Yanga SC na Watu ambao walikuwa na msaada mkubwa mno Klabuni akina Seif Magari na mwenzake Bin Kleb ' Watoto wa Mjini ' tupu na ambao ' Umafia ' wote wa Soka la Bongo walikuwa wanauweza ila Manji alipoona tu hawa Jamaa wawili wanaanza kukubalika mioyoni mwa wana Yanga SC akawatengenezea ' zengwe ' wakaanza kuchukiwa na wakaamua kukaa pembeni mwa Klabu / Timu.

Manji aliiharibu sana Yanga SC na kwa mifumo yake mobovu aliyoiweka itawachukua muda mrefu kidogo Yanga SC kuja ' Kusimama ' na angalau kuja kuwa kama Simba SC Kimikakati na Kimaendeleo. Siku nyingine nitakuja kutiririka na kuserereka zaidi juu ya Manji na hatma kamili ya Yanga SC lakini kwa leo naomba niishie hapa tafadhali.
 

Yanga inaweza kufanya mikakati na ikawa klabu kubwa barani Afrika...lakini kinachoisumbua Yanga ni kuendekeza majungu na kuruhusu 'kutawaliwa'....Watu wazima na akili zao wanalipiwa hata ada ya kadi, kwenye mkutano wanapikiwa pilau halafu eti wanaona hayo ndiyo maendeleo....Uswahili na umangimeza umezidi mno Yanga...hovyo kabisa...
 
Kuchanga sio tatizo na tim inaweza kwenda bila michango ikawa na vyanzo vengine tu vya mapato shida ni je pesa hizo zitafanya lengo husika la kuinua soka la yanga?
 
Acheni Kulialia na Kigenge Chenu Cha Maandazi!
Si Mwende tu Mukampigie Magoti na Kumlilia Manji Wenu!!!
 
Hivi sheria za soka zinaruhusu kumiliki timu VPL na kuwa mwanachama Wa klabu nyingine??Takukuru mechi ya Simba na Azam matokeo yalipangwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…