punyeto
punyeto ni tendo lolote la kujitafutia
ashiki binafsi hasa kwa kuchochea viungo vya uzazi. Wanaochukua hatua hiyo ili wajipatie kionjo cha kuridhisha kinachofanana na kile cha
tendo la ndoa kwa kawaida wanasukumwa na
msisimko uliowapata, pamoja na
haya ya kujitafutia mtu na
hofu ya kuambukizwa
maradhi ya zinaa.
tathmini mojawapo
kufanya hivyo ni kupotosha maana ya
jinsia kwa
binadamu, ambayo ni kufanya wawili wawe kitu kimoja kwa nguvu ya
upendo ambao uanze rohoni na kukamilika katika muungano wa miili yao.
Upendo maana yake ni kujitoa kwa muungano na mpenzi unaoleta tunda lake katika
mtoto, ambaye ni kwa pamoja wa
baba na wa
mama, akiwaunganisha upya ndani mwake.
Katika tendo la kujichua hakuna lolote kati ya hayo: Hakuna upendo wala kujitoa kwa wengine, hakuna muungano wala
uzazi, isipokuwa kujitafutia iwezekanavyo furaha ya kimwili (
ashiki) iliyokusudiwa na
mungu kuwa sehemu ya furaha nzima ya muungano wa ndoa.
Katika tendo hilo la
ubinafsi mtu yuko peke yake na kubaki peke yake: Halengi chochote nje ya
mwili wake, hivyo anazidi kuzama ndani mwake
badala ya kustawi kwa kujiwekea malengo mema (k.mf.
ndoa,
haki,
huduma kwa wenye shida,
utume n.k.). Matokeo yake ni kupoteza
nguvu za mwili na hasa kuvuruga msimamo wa
nafsi kwa kujisikia mnyonge, mwenye kosa na mtumwa wa tendo ambalo analikinai mara tu baada ya kulitenda. Hatimaye anaweza kupata matatizo katika tendo la ndoa.
Kwa msingi huo
kanisa katoliki linahesabu punyeto kuwa
dhambi kubwa, tena upande mmoja ni kubwa kuliko
uasherati (kuzini kati ya msichana na mvulana), kwa sababu linakwenda kinyume cha
maumbile na kuandaa njia kwa dhambi nyingine (k.mf.
ushoga).
Hata hivyo
elimunafsia inatueleza pia urahisi kwa mtu asiyekomaa kimapendo kufuata njia hiyo danganyifu, tena ngumu kuachwa baada ya kuzoeleka.
Ndiyo sababu
kanisa linamhimiza
padri kupokea kwa
huruma wenye tatizo hilo na kuwasaidia mashauri ya kibinadamu pia kuhusu afya ya mwili na ya nafsi. Kwa mfano: Kunyosha
viungo kwa
kazi za mikono au kwa
michezo, kulalia pagumu tena si kifudifudi, kukwepa vinywaji vinavyochochea
neva (
kahawa,
chai n.k.), kushirikiana zaidi na watu, kusaidia wenye shida. Upande wa roho awashauri kufuata vizuri
dini. Awatumainishe wanaweza kushinda, kwa hiyo wasikate tamaa wala wasiogope mno.
Punyeto imekatazwa kwa dini zote mbili yaani dini ya kiislam na dini ya kikristo kwa ushauri wangu bora uache kupiga hiyo punyeto na ukiendelea sana matokeo yake nguvu zako za kiume zitapunguwa hutaweza kumstarehesha mwanamke vizuri.