Jambazi sugu ajisalimisha kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya baada ya kukoswa koswa na risasi za Polisi

Ngoja nimpe binti mimba then nijisalimishe kwa mkuu wa wilaya yetu bhana aniachie mkee na mtaji wa kutosha kutunza mtoto au watoto ushauri nijaribu hili NAKWEDE
 
Yaani kakoswa na risasi za Polisi halafu anajisalimisha na kupewa milioni pamoja na pongezi juu du!

I wish I could be IGP
 
... in short polisi waliokuwa wakimtafuta "kwa muda mrefu sana" sasa wameshajua yuko wapi wakamchukue otherwise ni usanii juu ya usanii.
 
Safi sana. Anaeomba husamehewa hata na Allah seuse sisi binadam.

Namshauri kijana ashike swalat na asiache na Allah atamsameh.

Nawaomba na wale wote aliowakosea wamsameh.
 
"Ujasiri wake wa kujisalimisha umepongezwa na kamati ya ulinzi na usalama?
 
Aisee! yaani unakiri ulikuwa jambazi sugu, umefanya matukio mengi lakini unapewa hela badala ya kupelekwa polisi? Basi sawa. Sijui RC atampa ngapi na yeye? Hongera kwa kupata BIKO kijana.
 


Movie
 
Mahakamani anapelekwa lini?au kiki za uchaguzi maana CCM mna vijimambo.
Nadhani hafikishwi mahakamani na sidhani kama ni kiki za Uchaguzi kwa sababu tunaambiwa ''CCM hawana haja ya kufanya kiki ili wachaguliwe kwa sababu wanaiba kura''!

Huwezi kusema wanafanya kiki kwa sababu ya chaguzi halafu hapo hapo unasema huwa wanaiba kura!
 
Sasa tutaaminije hawaibi kama hakuna maigizo na sanaa kama hizi?
 
Insanity! Sasa kama kajisalimisha si apelekwe rumande kusubiri kesi? Kosa halina expiry date, hadi ulilipe. Sasa na milioni 1 juu? Na hivyo vyombo vya habari vilijuaje ataenda kujisalimisha siku hiyo?

Maigizo mengine ya kitoto sana.
Wazee wa kupingaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…