Mr DIY
JF-Expert Member
- Dec 24, 2016
- 1,188
- 2,553
Mwaka mmoja nilifika eneo moja hapo Morogoro, njia ya Dodoma kabla hujafika mizani, sasa mwenyeji wangu alinambia nikishuka kwa bajaji nichukue boda mpaka kwake, sasa kama kawaida bajaji umesimama tu boda kibao hizi hapa nikadandia moja chap nikampa maelekezo akaanza yafuata, barabarani jamaa akawa na story nyinginyingi si wajua tena boda, kufika mahali jamaa akasimamisha boda yake akaniomba nisimame pale nikimsubiri yeye aingie chocho moja na boda yake akidai anafuata ugolo wake huko, dah nikaona isiwe tabu nikashuka, nimesimama pale dk 3 jamaa hatokei, nikaona nidandie boda nyingine niendelee na safari, kama mwendo wa dk 5 hivi yule boda wa kwanza akawa aja mbio akitokea nyuma yetu na matusi kibao nishuke tuendelee na safari, sema yule boda nliokuwa nae alikuwa na msimamo wake, aisee ilikuwa rapsharapsha pale kidogo tudondoke teja boda kakomaa, kidogo akatokea mmama anaita boda basi ndio jamaa aka giveup, anyway nisiwachoshe na nyie tiririkeni hapa