Kama unajifunza kilimo fanya haya yafuatayo.
1. Lima eneo dogo la 20 x 20.
2. Chunguza aina za mboga za majani wanazotumia wanaokuzunguka.
3. Lima matuta saba marefu. Panda kwa kupishanisha wiki moja moja.
4. Weka mapapai matano ya kisasa. Manne pembezoni na moja katikati.
5. Dhibiti eneo kuku wasiweze kuingia kwa kuweka uzio. Tumia uzio unapatikana kwa bei nafuu, kama neti, mitende, makuti nk.
6.eneo liwe na jua la kutosha.
7. Tumia mbolea ya asili.
Faida zake
1.Utajifunza zao gani linakubali zao gani halikubali.
2. Utavuna kwa mzunguko. Na utapata matumizi nyumbani.
3. Wateja watakufwata wenyewe hutahitaji kujitangaza.
4. Utaweza kuihudumia kwa chini ya saa moja tuu kwa siku
5. Utapata mboga ya familia na kuokoa fedha.
6. Utajifunza kilimo na utaweza kukipanua au utashindwa na kama utakata tamaa utaacha.
7. Inafaa kuwafundishia watoto.
Hasara zake.
1.Bustani lazima iwe karibu na nyumbani
2. Utahitaji muda wa kuihudumia kila siku