Jambo la Muhimu ukiamua kufuata kilimo

Jesusfreak08

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2019
Posts
822
Reaction score
1,803
Kilimo kinafaida kama sheria zake zikizingatiwa kuna mambo usipo yazingatia kwenye kilimo basi nakuhakikishia utaambulia maumivu au hasara kitu kama ufuatiliaji kama hauna ufuatiliaji mzuri wewe binafsi au mtu anaye simamia basi hasara ni uhakika

—Kilimo kinafaida kikizingatiwa
 
Kila biashara inachangamoto sio kilimo tu, inategemea na ww umeingia vp ukiingia kichwa kichwa utaona wanaolima wt ni wa puuzi . Jambo la msingi kabla ujaanza fanya utafuti wa bidhaa unayotaka kulima kuanzia mbegu, usimamizi wa shamba, masoko n.k..., karibu shambani mzee.
 
Kilimo ni Cha kuvizia vizia Sana Mana hata soko lake halieleweki muda wowote kina kupiga ngumi za uso(Bei ndogo).
Bei inategemea na ubora wa bidhaa, ukuwa na mzigo mzuri bei nazo ni super ukifanya ujanja ujanja aaaah Bei nazo ni za ubabaishaji , mbona bakhresa anatengeneza biscuit za sh 50, inamaana yy hakuangalia Bei!?
 
Kama unajifunza kilimo fanya haya yafuatayo.
1. Lima eneo dogo la 20 x 20.
2. Chunguza aina za mboga za majani wanazotumia wanaokuzunguka.
3. Lima matuta saba marefu. Panda kwa kupishanisha wiki moja moja.
4. Weka mapapai matano ya kisasa. Manne pembezoni na moja katikati.
5. Dhibiti eneo kuku wasiweze kuingia kwa kuweka uzio. Tumia uzio unapatikana kwa bei nafuu, kama neti, mitende, makuti nk.
6.eneo liwe na jua la kutosha.
7. Tumia mbolea ya asili.

Faida zake

1.Utajifunza zao gani linakubali zao gani halikubali.
2. Utavuna kwa mzunguko. Na utapata matumizi nyumbani.
3. Wateja watakufwata wenyewe hutahitaji kujitangaza.
4. Utaweza kuihudumia kwa chini ya saa moja tuu kwa siku
5. Utapata mboga ya familia na kuokoa fedha.
6. Utajifunza kilimo na utaweza kukipanua au utashindwa na kama utakata tamaa utaacha.
7. Inafaa kuwafundishia watoto.

Hasara zake.
1.Bustani lazima iwe karibu na nyumbani
2. Utahitaji muda wa kuihudumia kila siku
 
Faida number 8. Utaiona faida ya Muda ni mali.badala ya jionkwenda kupata moja moto moja baridi wewe muda huo utakua bustanini ukihudumia bustani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…