Uncle Mabiki
Member
- Sep 22, 2018
- 77
- 77
Asante kwa wewe ulieingia kwenye huu uzi,ili kufahamu ni jambo gani hasa lililobeba maono ya Tanzania ijayo. Kwanini ni jambo ambalo nimelipa jina la hisia basi karibu na tiririka mpaka mwisho
Kwa takribani miaka 50 Tanzania imepitia mifumo mbalimbali ya uongozi na uendeshwaji, pamoja na hayo tumeshuhudia ujamaa, ubinafsishaji n.k.
Ilichukua miaka 28 tu mfumo wa vyama vingi kuingia mwaka 1992 toka Tanganyika na Zanzibar ziungane mwaka 1964, yani miaka 28 toka mwaka 1964 mpaka 1992, kwanini miaka 28 tu, kwasababu ya hisia.
Hisia zilitufanya tutafute mtu ambae ni mkweli na atatutoa kwenye dimbwi la umasikini tulilotumbukizwa enzi za ukoloni. Miaka imepitia na kupita, maraisi wamepita na kupita, je watu ambao tunawapa kijiti watuokoe toka kwenye hisia mbaya vichwani mwetu na mioyo yetu, je wamefanikiwa au laah.
Mbona hisia zetu zinatuambia Bado sana, tulivyokuwa na tulipo ndo vilevie, maana tunafiwa na ndugu zetu wapendwa kwa uhaba wa vifaa hospitalini, tunapata huduma nusu hospitalini huku mzigo wa dawa tunapewa sisi kununua, Je vipi kuhusu watoto wetu mashuleni, ambapo asilimia 80 ya makuzi yao yapo shuleni, je kuna Walimu wa kike wa kutosha kusaidia watoto wa kike, je kuna Walimu wa kiume kuwaelewa watoto wa kiume, sikuizi wezi, majambazi, wanaojiuza wanatokea mashuleni.
Na vipi kuhusu maisha ya watanzania wote, je hisia zao kuhusu afueni ya maisha ipoje kwao, ajira kwa vijana, utelekelezaji wa mikopo kwa vijana mbona zinasikika tu TBC2 lakini vijana wenyewe mtaani hawapati, au mgawaji anagawia anaowajua na si wanaohitaji kugawiwa
JE NINI KIFANYIKE KWA TANZANIA YA KESHO
Mimi na wewe unahisi nini kifanyike, hapo nazungumzia hisia
1. kwanza tunahitaji mtu Bora wa kutibu hisia zetu, mtu mwenyewe ni kiongozi, mtu atakaeweza kutibu nyongo na mioyo ya watanzania, kiongozi huyo atambue kuwa Watanzania tunamateso yanayotusibu, na atambue kuwa uongo hauwezi tibu kitu, kama akimdanganya baba, je mtoto wake akikuta Bado kifuatacho ni mtafaruko na machafuko yasiyoisha
2. Pili Tanzania ya kesho inahitaji mfumo Bora na madhubuti wa kuendana na Dunia sasa, maana hauwezi tumia mfumo wa enzi za nuhu kwa Dunia ya sasa, mfumo wenye mabadiliko na maboresho ili kusaidia mfumo uliopo sasa, unaweza pata kiongozi Bora kwa sasa ila kupitia mfumo alioukuta akawa tapeli, na mdanganyifu, inatakiwa mfumo umbane kama tunavyowabana watoto mashuleni kuwa akiiba mtihani Shule hana
3. Na tatu kwa maneno mafupi sana Tanzania ni nchi yetu sote, wapo waliokwisha kufa walitamani kuiona TANZANIA yenye miundombinu Bora, elimu Bora, Tanzania yenye afya Bora, na Maisha Bora kwa ujumla, ewe nchi yangu Tanzania naamini vikifatwa hivyo vitu naiona Tanzania mbali.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA
NA WATU WOTE DUNIANI
Upvote
1