James Comey ameandika kwenye Instagram 8647; je anaashiria nini?

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
9,818
Reaction score
14,585





Aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani wa FBI, James Comey alichapisha picha kwenye Instagram ikionyesha magamba ya bahari yakiwa yamepangwa kuunda namba 8647. Baada ya chapisho hilo, kulikuwa na mjadala mkubwa mtandaoni, hasa kutoka kwa wahafidhina, wakidai kuwa namba hizo zinaweza kuwa na maana ya kisiasa au hata tishio dhidi ya Rais Donald Trump

Kwa mujibu wa kamusi ya Merriam-Webster, namba 86 mara nyingi hutumiwa kumaanisha "kuondoa" au "kutupa nje," na 47 inahusiana na Trump, ambaye ni rais wa 47 wa Marekani. Baada ya malalamiko kuongezeka, Comey alifuta chapisho hilo na kueleza kuwa hakutambua kuwa namba hizo zinaweza kufasiriwa kama ujumbe.

Hili limepelekea uchunguzi kutoka kwa Idara ya Usalama wa Ndani na Huduma ya Siri ya Marekani. Comey amesisitiza kuwa hakumaanisha chochote kibaya, lakini mjadala kuhusu maana ya namba hizo unaendelea.
 
Huduma ya Siri ndio secret service?
 
Huduma ya Siri ndio secret service?
 
Ukiwa Shushushu, maadili ya kishushushu hata kama umestaafishwa au umestaafu, utulie kimya, la sivyo utatulizwa moja kwa moja for good..!!
 
Na amefuta kabisa akaunti yake ya insta. Ikumbukwe kuwa huyu alikuwa na bifu na Trump toka zamani hadi Trump katika awamu yake ya kwanza akamwondoa kwenye nafasi ya boss wa fbi
 
Kumbe Wazungu nao wanaongeaha kimafumbo?

Hapo anamaanisha namba ya chumba chake anakopelekwa kwenye gereza matata la Alcatraz, analofungua upya Trump.
 
Hakuna aliyewahi kuhojiwa juu ya jaribio la kumuuwa Tundu Lissu Dodoma kwenye makazi ya viongozi area D. Siku hiyo hiyo cctv camera zilizokuwa nyumbani kwa Karemani ambaye alikuwa Jirani yake ziliondolewa
 
Lazima anayo sababu ya kupost hvyo
Donald Trump alimfuta kazi James Comey, Mkurugenzi wa FBI, Mei 9, 2017, kwa sababu za kisiasa na za kibinafsi. Rasmi, Trump alidai Comey alishindwa kusimamia FBI vizuri, hasa kuhusu uchunguzi wa emails za Hillary Clinton. Lakini wengi wanaamini Trump alitaka kumdhibiti Comey kwa sababu ya uchunguzi wa FBI kuhusu uhusiano wa kampeni yake na Urusi, ambao ulionekana kama tishio kwa uongozi wake. Comey alikuwa akiongoza uchunguzi huu, na Trump alihisi shinikizo. Uamuzi huu ulizua mzozo mkubwa, ukiashiria mgogoro kati ya utawala wa sheria na maslahi ya kisiasa ya Trump.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…