James Kotei atua DTB

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
James Kotei aliyekuwa kiungo wa zamani wa Simba amesajiliwa rasmi na timu daraja la kwanza DTB ,hii club huko daraja la kwanza haishikiki ikiwa na wachezaji wakubwa tu Kama kina Hamis Tambwe,bila shaka itapanda daraja msimu huu.

Swali ni kwamba ligi yetu imekuwa juu sana hadi wachezaji wakubwa wanakosa timu za ligi kuu wanaenda daraja la kwanza?
 
Hongereni sana DTB kwa usajili wenu wa kutisha. Naamini mtaleta ushindani wa kutosha sana kwa Mabingwa watarajiwa wa ligi kuu (Yanga), msimu ujao.
 
Timu ikipanda daraja wachezaji wanachukuliwa simba na yanga wanakaa benchi na ndio unakuwa mwisho wao huo wanashuka daraja hii ndo Tanzania.
 
Bongo kuna bata sana amin usiamin,hao wachezaji wa nje wakionja life ya bongo wako tayari kucheza hata daraja la nne,muulize niyonzima,chirwa,tambwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…