James Mbatia: Tunatoa pole kwa CCM kuondokewa na kada wao Hamza katika mazingira ya ajabu

James Mbatia: Tunatoa pole kwa CCM kuondokewa na kada wao Hamza katika mazingira ya ajabu

pakaywatek

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
4,660
Reaction score
6,282
"Sisi NCCR-Mageuzi tunatoa pole kwa polisi waliouawa juzi, tunatoa pole za dhati kwasababu ni binadamu, wametoa uhai wao. Tunatoa pole kwa familia ya Hamza pia kwasababu huyu ni binadamu, wasiendelee kujenga chuki, tunatoa pole kwa wote, roho za binadamu zilizoondolewa.

Tunatoa pole kwa chama cha Mapinduzi kwa kuwa Hamza alikuwa kada wa chama cha mapinduzi. Si wakubali tu! Unaweza ukawa na watoto, mtoto mwingine hayuko vizuri lakini ni binadamu, kwanini wanakataa Hamza sio mwanachama wao, ni mwanachama wao, ni kweli amefanya tukio hilo wakubali, wajiangalie, wajitazame upya kwanini mambo hayo yanatokea.

Ndio maana sisi tunatoa pole kwa chama cha mapinduzi kwa kuondokewa na kada wao, ndugu Hamza katika mazingira ya ajabu sana"

James Mbatia
Mwenyekiti-NCCR Mageuzi

Mbatia.jpg
 
Ila usikute Yale mafunzo kayapata kwenye mambo ya Green Gurd
Sasa unadhani wapi mkuu?ndo hukohuko.Kuna ndugu yangu alikuwaga green weeee!hayo mambo alikuwa ananiambia ni hatari.Hakuna watu wanajiamini Tanzania kama green guard sijui huwa wanaambiwa nini huko kuhusu Tanzania na watu wengine ambao si ccm?
 
Hamza hakuwa tu kada wa CCM, lakini alikuwa pia kiongozi wa CCM. Chama kimeondokewa na nguzo mojawapo ya chama.
 
Hamza hakuwa tu kada wa CCM, lakini alikuwa pia kiongozi wa CCM. Chama kimeondokewa na nguzo mojawapo ya chama.
Alikuwa pia akifadhili baadhi ya miradi ndani ya chama. Tumempoteza mtu muhimu sana kwenye chama chetu ccm
 
Back
Top Bottom