James Mbowe amwaga pongezi kwa ATC 'Any Time Cancellation'

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,155
Reaction score
2,704



Nichukue nafasi hii kipekee kuwapongeza Air Tanzania kwa namna wanavyo badili ratiba za ndege mara kwa mara. Mfano leo ndege ya Air Tanzania iliyokuwa iruke kwenda Kigoma saa 5:40 imesogezwa mpaka saa 9:30 sababu wanasema ni Operation yaani siyo hata kwamba hali ya hewa ni mbaya au ndege mbovu bali ni sababu za Uendeshaji.

Yaani mnaacha Abiria wanatoka majumbani usiku wanawahi Airport alafu kwa Urahisi kabisa bila Aibu mnatangaza ni sababu za kiuendeshaji.

Kwa kweli kutoka Moyoni niwapongeze sana hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Shirika letu linavyowajali wateja wake. Kuna mtu aliwahi kuniambia Kirefu cha ATC ni Anytime Cancelation, sasa nimeanza kumwelewa.
 
Ni sahihi,wanapaswa kupongezwa!
Ukikosoa na kutoa mawazo tofauti Girishoni anakushighulikia🤣🤣🙃🙃🙃
 
Haya ya kufufua shirika yalikuwa maono ya mtu mwingine.
Amekufa nayo March 2021.
Unafikiri wakati wake angeendelea kuvumilia uhujumu shirika kama huu?
 
Nikiona Mtu analalamika mtandaoni kwa sababu Ndege imechelewa.Huwa namshangaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…