Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Kocha wa timu ya Mwadui FC Jamhuri kiwhelu ‘Julio' ametua timu ya Coastal Union hadi mwisho wa msimu huu.
Kocha huyo mwenye maneno mengi, ameiwezesha timu ya Mwadui kupanda daraja kushiriki ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
Coastal Union imekuwa na matokeo mabaya msimu huu kwenye ligi kuu ya Vodacom hivyo imelazimika kumchukua kocha huyo ‘kwa mkopo' ili aweze kuinusuru timun hiyo kongwe isiteremke daraja.
Tayari African Sport timu nyingine ya Tanga imepanda daraja baada ya zaidi ya miaka 20, iwapo Coastal Union itabaki ligi kuu, timu hizo zenye upinzani wa jadi zikarudisha hamasa ya soka mkoani Tanga.
Chanzo: Habari247